Ufahamu wa Sayari kwa Kutumia Universe in a Box

20141015_115831Shule ya msingi Ilboru ni baadhi ya shule za kwanza kabisa nchini Tanzania kuweza kupata na kutumia vifaa vya kufundishia sayansi kutokana na programu ya UNAWE. Vifaa vya aina mbali mbali vinajulika kama Universe in a Box, kwa kupita Mwalimu Eliatosha Maleko wanafunzi wa shule hii wameweza kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo na kuongeza udadisi na shauku ya kufahamu zaidi.

Wanafunzi hawa na mwalimu wao hupenda kushikirisha jamii kwa kile wanachojifunza na kufanya ili kuleta shauku na changamoto katika jamii juu ya njia bora ya kujifunza sayansi. Na leo hii wanatuambia na kutuonyesha ni kwa namna gani wemeweza kujifunza kuhusu sayari na mfumo wa Jua kwa kutumia vifaa vya Universe in a Box au Ulimwengu katika Box kwa Kiswahili.

20141015_113816Katika mada hii wanafunzi wamejifunza mambo mbalimbali yaliyoko angani zikiwamo sayari zote tisa (ukijumuisha sayari ndogo ya pluto) kama inavyoonekana katika picha walizopiga pamoja na michoro waliyo nayo. Pia wameweza kufahamu umbali uliopo toka sayari moja na nyingine pamoja na muundo mzima wa sayari moja na nyingine.

Hata hivyo wanafunzi hawa wamefurahishwa sana na somo hilo la anga pamoja na vifaa walivyopewa na wafadhili, ambapo katika mada hiyo wanafunzi hawa wameelewa na wameuliza maswali mbalimbali kama vile.

Je? ukienda katika sayari ya Saturn unaweza kushika ile pete? na je hiyo pete imeundwa na nini?, kupatwa kwa Jua au mwezi kunatokeaje na nini madhara yake katika maisha ya binadamu.

Kama una ufahamu au majibu ya maswali haya basi wanafunzi na mwalimu wao wengependa kusikia toka kwako kwa kucomment kwenye mada hii hapo chini.

Kwa pamoja tunaleta sayansi kwa watoto wa Tanzania.

20141015_112522

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s