Uhusiano wa Maisha na Mazingira Yetu

Ni wazi kuwa maisha katika uso wa Dunia hutegemea huduma ubora wa huduma zitolewazo na mazingira husika. Ukiangalia mfumo wa ikolojia wa misitu, bahari, mbugani na kwenye udongo utaona uwepo wa maji, hewa nzuri na rutuba ya udongo ndivyo vinavyopelekea wanyama na mimea kuwepo na kupendezesha mazingira.

20140324_115334Wanafunzi wa shule ya msingi Ilboru walipata nafasi ya kujifunza kuhusu uhusiano ulipo kati ya mazingira na maisha ya viumbe hai katika uso wa Dunia. Waliweza kutambua kuwa Mazingira  ni jumla ya mambo yote yanayotuzunguka ikijumuisha viumbe hai na vile visivyo hai. Viumbe hai ni pamoja na binadamu, wanyama na mimea na vile visivyo hai ni pamoja na hewa, Jua, udongo.

HEWA – ni sehemu muhimu ya mazingira kwani viumbe hai vyote hupumua ili kumudu maisha. Wakati wanyama wanavuta hewa ya oksijeni mimea huvuta hewa ya Kaboni dayoksaidi wakati wa mchanga ili kutengeneza chakula, hewa ambayo wanyama huitoa kama hewa chafu. Hapa tulijifunza uhusiano kati ya wanyama na mimea katika kuishi na pia katika kuweka usawa wa hewa safi angani.

UDONGO – ni maada ambamo mimea hupandwa na kukulia pia wanyama hupata mahitaji yao kama Chakula kutoka kwenye udongo na pia udongo hufanya nchi kavu ambapo binadamu na Wanyama wengi huishi. Lakini pia udongo unahifadhi wadudu wadogo wadogo wengi tusioweza kuwaona kwa macho ambao husaidia kurutubisha udongo na kuifanya mimea iweze kustawi na pia mizizi iweze kupata maji na hewa. Hapa tunaona umuhimu wa udongo katika kuboresha maisha kwa kuifanya mimea iweze kukua.
JUA – ni chanzo kikubwa asilia cha nishati ya mwanga na joto. Nishati ya mwanga kutoka katika Jua mbali na kutupatia joto na kusaidia kufanyika kwa mvua na kupunguza baridi katika uso wa Dunia, bado ni muhimu sana katika kuisaidia mimea kuweza kutengeneza chakula chake chenyewe. Bila kuwepo kwa mwanga wa Jua mimea itashindwa kutengeneza chakula na kupelekea kufa, hivyo kuwafanya wanyama wanaotegemea mimea kufa, ambao nao watawafanya wanyama wala nyama kufa akiwamo binadamu anayekula nyama na mimea.
MAJI – yamechukua sehemu kubwa ya Dunia yetu, ni sehemu kubwa ya miili yetu na maisha ya viumbe wengi hutegemea maji kwa ajili ya kuwa hai. Maji hupatikana katika maeneo mbali mbali kama kupitia mvua na hupatikana kwa wingi katika mito, maziwa, visima, bahari, barafu ,unyevu na Umande na pia chini ya ardhi. Maji huzunguka kwa kuvukizwa kutokana kwenye uso wa Dunia na kupanda juu na kutengeneza mawingu ambayo baadae hurudi Duniani kama mvua au theluji na kufanya maisha yaendelee Duniani.
20140513_131002
Mvua inaponyesha kiasi kikubwa cha maji yake huanguka ardhini na kisha kuzama chini na kufanya Chemchem, maji yanayotiririka hufanya Mito nayo mito hutiririka hadi katika maziwa au Bahari kisha maji ya bahari yanapopata joto mtiririko hujirudia.
KUTEGEMEANA KATIKA MAZINGIRA (IKOLOJIA) – Viumbe hai vimegawanyika katika makundi mawili nayo ni  Mimea na Wanyama. MIMEA hutegemea mazingira ufu na ndilo kundi pekee lenye kujitengenezea chakula chake chenyewe kwa kutumia chumvichumvi za ardhini, maji,gesi ya kabon dayoksaid na mwanga wa jua na kufanya mimea kukua katika udongo au maji. Mimea bado hutegemea wanyama kuweza kustawi kutokana na samadi inayotokana na wanyama kisha huoza na kufanyika mbolea inayorutubisha udongo.
Mzunguko wa Nishati
WANYAMA hutegemea kupata hewa safi ya oksijeni iliyotengenezwa na mimea, ambayo hutumika kutengenezea  nishati kutokana na chakula kilichosharabiwa katika mwili.
MZUNGUKO WA KABONI – hutokana na kutegemeana kwa viumbe hai kwa ni Kabonidoiksaidi iliyoko hewani ambayo hutumika na mimea kutengeneza chakula. Mimea huliwa na baadhi ya wanyama kisha wanyama hao huliwa na wanyama wanaokula nyama.kisha mizoga ya wanyama na mimea huoza na kutoa kaboni inayorudi angani
Katika mada hii wanafunzi walionyesha udadi wao kwa kuuliza maswali ya kutaka kujua zaidi, mfano
Je ni nini kitatokea iwapo Jua litakoma kuwaka?
Je ni nini kitatokea iwapo wanyama wanaokula nyasi wakiliwa na kuisha?
Je simba,chui,fisi na wengine watakula nini?
Unaweza kusaidia kutoa majibu ya maswali haya na kushiriki kujifunza pamoja na wanafunzi wa Ilboru.
Imeandaliwa na Mwalimu Maleko
Advertisements

One thought on “Uhusiano wa Maisha na Mazingira Yetu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s