UNIVERSE IN A BOX DARASANI

Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Ilboru wanayofuraha kubwa kuweza kupata vifaa vya kujifundishia kutoka UNAWE. Vifaa hivi kwa ujumla vinaitwa Universe in a Box ambapo ndani yake kuna vifaa mbali mbali vya kujifunza mada za sayansi.

Kwa kutumia vifaa hivi wanafunzi waliweza kujifunza kwa urahisi mada ya mfumo wa Jua na kuweza kutambua kwa urahisi sifa za sayari zipatikanazo ndani yake ambazo ni Zebaki, Zuhura, Dunia, Mirihi, Sumbula, Sarateni, Zohari na Kausi. Pamoja na Jua sayari hizi hutengeneza kitu kinachojulikana kama Mfumo wa Jua.  Sayari zote hizi huzunguka Jua lililopo katikati ya mfumo huo na pia hutapa nishati ya mwanga na joto.

Mbali na kufahamu tabia na sifa za sayari hizi wanafunzi waliweza kuelewa umbali uliopo baina ya sayari hizo huko angani.

 1. 20140331_114624Sayari ya Zebaki umbali  wa km 58 milioni na huchukua muda wa siku 88 kulizunguka Jua
 2. Sayari ya Zuhura umbali wa km 108(mill) na huchukua siku 225 kulizunguka Jua
 3. Dunia iko umbali wa km150milioni na huchukua siku 365 na robo au 366 kuzunguka Jua
 4. Mirihi umbali wa km milioni 228 na huchukua muda wa mwaka 1 na siku 322 kulizunguka Jua
 5. Sumbula iko umbali wa km milioni 778 na huchukua miaka 11 na siku 314 kuzunguka Jua
 6. Sarateni iko umbali wa km milioni 1426 na huchukua miaka 29 na siku 168 kuzunguka Jua
 7. Zohari iko umbali wa km milioni 2868 na huchukua miaka 84 kuzunguka Jua
 8. Kausi iko umbali wa km milioni 4495 na huchukua miaka 164na siku 282 kulizunguka jua.

Wanafunzi waliweza kufahamu kuwa uwapo wa sayari ya Dunia katika umbali kwa km milioni 150 kutoka kwenye Jua, unaiwezesha kuwa na sifa ya makazi ya mimea na viumbe hai kuliko kwenye sayari nyingine.

Ukichukulia mfano sayari ya Zebaki na Zuhura ambazo zipo karibu kabisa na Jua joto ni kali sana ukilinganisha na lile linalofika Duniani,wakati zile zinazopatikana mbele ya sayari yetu zina hali ya baridi kali ukilinganisha na lile la Duniani. Jambo linalofanya uwepo wa maisha kama tunavyoyafahamu sisi kushindikana, katika sayari hizo.

Wanafunzi waliweza pia kufahamu kuwa Zebaki ni sayari ndogo kuliko zote ikifuatiwa na sayari ya Zuhura na kuwa sayari hizi zipo karibu sana na Jua. Sayari  ya Zuhura pia inaweza kuonekana kwa macho wakati wa usiku kwani ina wingu kubwa na pia hung’aa sana wakati wote hasa kabla ya Jua kuchomoza na hivyo kuitwa nyota ya asubuhi.

Wanafunzi waliweza kuelewa kuwa pamoja na Dunia yetu kuwa na Mwezi mmoja unao izunguka sayari nyingine pia zina miezi inayozizunguka ambapo:-

 • Sayari ya Sarateni ina miezi 9  na imezungukwa na Pete kubwa ambayo ni miamba midogo midogo, barafu na wawe.
 • Sayari ya Mirihi ina miezi 2 midogo
 • Sumbula ni ambayo ni sayari kubwa kuliko zote ina jumla ya miezi 12 na zaidi.

Mwisho tunawakaribisha kujifunza pamoja nasi elimu hii ya sayansi ili tuweze kupata ufahamu zaidi.

Imeandikwa na Mwl. E. Maleko

Ilboru Shule ya Msingi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s