Wanafunzi Ilboru Wajifunza Tabia ya Nchi kwa Zana

Wanafunzi wa shule ya Ilboru wameweza kujifunza mada inayohusu tabia ya nchi katika somo la Jiografia. Pia wanapenda kueleza kwa ufupi kile walichojifunza kuhusiana na mada hiyo pamoja na kuelezea kuhusu vitu vinavyoathiri na kupelekea tabia ya nchi katka mahali fulani.

20140318_131459Tabia ya nchi ni wastani wa vipimo vya hali ya hewa vinavyochukuliwa kila siku katika kipindi cha miaka 25hadi 30. Vipimo hivi huusisha, mvua, jotoridi, upepo, mawingu, pamoja na unyevu. Hivyo basi tabia ya nchi inatupatia picha nzima ya hali ya hewa katika maeneo mbali mbali Duniani. Mfano ni maeneo fulani kuwa na mvua nyingi au baridi sana katika vipindi tofauti tofauti vya mwaka.

Pia tumeweza kujifunza kuwa tabia ya nchi inaweza kutambulishwa na vitu mbali mbali kama vile,kiasi cha mvua, jotoridi, kasi ya upepo, unyevu na mawingu. Hata hivyo kuna mambo mbalimbali yanayoathiri tabia ya nchi kama vile- mahali eneo linapopatikana katika Dunia, mwinuko kutoka usawa wa bahari, mgandamizo wa hewa, misitu na kuwapo kwa maeneo makubwa yenye majimaji kama vile bahari au maziwa.

TABIA YA NCHI YA AFRIKA YA MASHARIKI NA VITU VINAVYOIATHIRI

Eneo kubwa la Afrika ya mashariki linapatikana ndani ya mstari wa kubuni wa tropiki ya kaprikoni na kupitiwa na mstari wa Ikweta unaoigawa Dunia katika sehemu sawa mbili, ambazo ni kizio cha kaskazini na kusini.

20140318_131612Afrika mashariki inapatikana kati ya latitudo 5 kaskazini na12 kusini mwa Ikweta ambalo ni eneo la ukanda wa tropiki wenye sifa ya kuwa na tabia ya nchi yenye joto. Ukanda huu  unaanzia Latitudo 0-23 kwa upande wa kaskazini na kusini mwa Ikweta.

Tabia ya nchi ya ukanda huu huathiriwa na mwinuko kutoka usawa wa habari, ukaribu na bahari au maziwa, misitu pamoja na pepo za misimu. Wastani wa nyuzi joto katika ukanda huu ni nyuzi 27c, ambapo kiwango hiki hutegemeana na mahali eneo husika lilipo

Kwa kutumia tufe la Dunia lenye mistari ya kubuni na lile lisilokuwa na mistari ya kubuni pamoja na atlasi, mwalimu wetu aliweza kutuonyesha mistari mbalimbali ya kibuni inayogawanya Dunia kama vile Tropiki ya Kansa, Kaprikoni na Ikweta.

Tuliweza pia kujifunza kuhusu Jua la utosi ambapo mfano kiasi cha jotoridi kinatokana na mabadiliko ya mahali Jua linapokuwa la utosi kaskazini na kusini mwa Ikweta. Jua huwa la utosi tarehe 21 Machi na 23 Septemba kwenye mstari wa Ikweta ambapo wakati huo mionzo ya jua huweza kuifika Dunia nzima na muda wa usiku na mchana hulingana. Tarehe 21 Juni Jua huwa la utosi katika Tropiki y Kansa katika latitudo 23 na nusu Kaskazini na 22 Desemba  Jua huwa la utosi katika tropiki ya Kaprikoni katika kizio Kusini latitudo 23 na nusu kusini mwa Ikweta.

Tunashukuru sana kwa kusoma makala yetu na tunakaribisha maoni yatakayofanikisha kujifunza kwetu masomo na mada mbalimbali, kwani elimu ni bahari na haina mwisho.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s