Sayansi ya Mmeng’enyo Wa Chakula

20140123_115656Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilboru kitengo maalum cha wenye ulemavu wa kusikia pamoja na walimu tunayo furaha kubwa na tunamshukuru Mungu wetu kwa kutupa tena mwaka mpya wa 2014, kwa pamoja tunapenda kushirikiana na wanafunzi wengine duniani katika kujifunza na kuonyesha uwezo wetu katika mambo mbalimbali kama masomo,michezo nk.

Katika makala hii tunapenda kuonyesha ni kwa jinsi gani tumejifunza somo la Sayansi katika mada ya mmeng’enyo wa chakula kama ifuyavyo:-

Mmengenyo wa chakula ni kitendo cha chakula kuvunjwa vunjwa kutoka katika hali tata na kuwa katika hali rahisi inayoweza kumezeka. Mfumo wa mmengenyo unahusisha ogani au viungo mbalimbali vya mwili ambavyo ni :-

20140123_124017Mdomo(kinywa), Umio/koo, Tumbo,Utumbo mdogo, Utumbo mkubwa(mnene) na Puru. Mwalimu aliweza kutufundisha ni kwa jinsi gani ogani hizi zinafanya kazi kwa kushirikiana kuanzia mdomoni na hadi kinapotoka katika puru.

Mdomo(kinywa) hupokea chakula ambapo huchanganywa na mate kwa kutumia ulimi na kisha kusagwa kwa kutumia meno ili kiweze kumezwa kwa urahisi. Katika mate kuna kimengenyo kinachoitwa Pitalini ambacho kina uwezo wa kubadili wanga kuwa katika sukari rahisi au glucose ambayo ni aina ya maltosi.

Baada ya kumezwa chakula kilichomengenywa hupita katika umio/koo la chakula na kumengenywa zaidi kabla ya kufika katika mfuko wa chakula ambao unajulikana kama tumbo.

Katika tumbo chakula hukaa kwa muda wa masaa matatu au zaidi kutegemeana na aina ya chakula mtu alichokula. Hapa chakula humeng’enywa zaidi kwa kutumia chachu zinazotolewa na tezi zilizopo tumboni. Moja kati ya  tezi hizo hutoa chachu inayoitwa gastriki ambayo inabeba kimengenya kinachoitwa (Pepsin) chenye uwezo wa kugeuza protini kuwa pepton, ambapo pia kuta za tumbo hutoa asidi inayojulikana kama Hydrocloric acid, ambayo kazi yake ni kuuwa vijidudu vinavyokuwa katika chakula.

20140124_113114Utumbo mdogo(mwembamba) hupokea chakula kinachotoka tumboni na kumalizia kazi ya kukimeng’enya na kukifyonza katika kuta zake kupitia vilas kwa ajili ya kusharubu chakula na virutubisho ili viweze kufika katika sehemu mbali mbali za mwilini na ogani zake. Utumbo huu  mwembamba ndio ogani ndefu kuliko zote katika mfumo wa mmengenyo wa chakula ambapo vimeng’enya vifuatavyo hupatikana:-

(a)Amylase – humeng’enya vyakula vyenye asili ya wanga.

(b)Lipas – humeng’enya vyakula vyenye asili ya mafuta na kuvigeuza kuwa, glicerol au asidi za mafuta.

(c) Taipsin – humeng’enya na kubadilisha Pepton kuwa asidi za amino.

Chakula kitokacho katika mtumbo mdogo huingina katika Utumbo mpana ambapo maji na madini mbali mbali husharabiwa. Kazi nyingineni ni kuhifadhi mabaki ya chakula ambacho hakijasharibiwa na kutolewa nje ya mwili kila baada ya muda fulani kupitia puru(anus).

Wisho kabisa tunapenda ketengeneza uhusiano na ushirikiano katika kujifunza zaidi kuhusiana na masuala ya sayansi na pia kubadilisha ujuzi baina yetu na wewe. Sisi Ilboru tunsema Sayansi ni dira katika maisha yetu ya kila siku na Mungu atubariki sana katika kuifahamu zaidi na kuitumia kwa manufaa yetu na viumbe wengine.

This slideshow requires JavaScript.

Imeandikwa na: Mwl. Maleko Eliatosha wa Shule ya Msingi ya Ilboru

Imehaririwa na: Mponda Malozo

Advertisements

One thought on “Sayansi ya Mmeng’enyo Wa Chakula

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s