Ulimwengu Mfukoni Mwako

Pocket_guide_translations-001Katika jitihada za kuifanya elimu ya astronomia kuwa rahisi na shirikishi kwa watoto, walimu na jamii nzima UNAWE-Tanzania ikishirikiana na EU-UNAWE wameweza kutengeneza kitabu kidogo cha mfukoni cha mazoezi.

Kitabu hiki kinachopatikana katika lugha kumi na saba (17) tofauti ikiwamo Kiswahili kinalenga kumsaidia mtumiaji kuchunguza anga la usiku, kudadisi na kutengeneza nadhalia mbali mbali ya vitu mbali mbali vipatikanavyo katika anga.

Kitabu hiki kikitumika ipasavyo kinaweza kuibua vipaji mbali mbali kama uchoraji, kutengeneza dhahania, kuwasilisha mawazo katika mfumo wa maandishi, picha au hadithi na pia kinaweza kujenga uwezo wa mtumiaji katika kufanya tafiti.

Kitabu hiki pamoja na matufe yanayoonyesha sayari ya Dunia bila mipaka na mistari mingine ya kufikirika iliyotengenezwa na binadamu vitasambazwa katika shule 20 zenye vilabu vya sayansi vilivyoanzishwa na UNAWE-Tanzania na unaweza kupakua nakala yako ya PDF hapa  au kwa kuwasiliana na coordinator kupita ukurasa wetu wa mawasiliano.  

EU_UNAWE_Earth_Ball

Advertisements

One thought on “Ulimwengu Mfukoni Mwako

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s