ILBORU NA MFUMO WA JUA

Jumla ya wanafunzi 65 wa darasa la tano katika shule ya msingi ilboru waliweza kushiriki katika mafunzo kwa vitendo juu ya mada iliyohusu mfumo wa jua pamoja na aina mbalimabli za sayari zilizoko angani.

Arusha-20130718-00359Katika mafunzo hayo wanafunzi waliweza kujifunza na kufahamu kuwa:-

Jua ni nyota iliyopo karibu zaidi  na sayari yetu ya Dunia kuliko nyota nyingine zote. Kuwa karibu na Dunia kumesababisha nuru au miale yake kuleta joto na mwanga katika uso wa dunia  kuliko nyota nyingine tunazoziona.

Nyota hiyo ya Jua ipo umbali wa Kilometa Milioni 149.6 kutoka katika Sayari yetu ya Dunia. Pia zipo  nyota nyingine angani ambazo ni kubwa kuliko Jua nyota hii na zina mwanga mkali kuliko ule wa Jua.

Uang’avu wa Jua unatokana na anuali za  kemikali na mwanga wa Jua huweza kutufikia Duniani kwa njia ya mnunurisho kwa muda wa dakika 8 na nusu tuu, ambapo mwanga wa nyota nyingine huchukua muda wa  miaka kadhaa kufika duniani.

Zaidi ya Jua kuna magimba mengine angani, Magimba haya ni Sayari, Asteroidi, na Mwezi.

Katika usiku mwang’avu usio na mawingu unaweza kuona vitu mbali mbali angani vikiwamo Mwezi na Nyota.

Nyota huwa ni ndogondogo na huonekana kama nukta zinazong`aa au kumweka, ambazo hutoa nuru za rangi Nyekundu,Njano au Bluu.

Pia wakati mwingine hasa wakati wa usiku,ukiangalia angani unaweza kuona nukta za nuru, ambazo huwa angavu, kubwa kwa umbo na hazimweki. Hizo huitwa Sayari.

Arusha-20130718-00358Je nitazitambuaje Sayari Angani? au Nini tofauti kati ya Sayari na  nyota?

Tofauti iliyopo ni kwamba,  nyota humweka na nuru yake haitulii,wakati nuru ya Sayari imetulia na haimweki ,Nyota huonekana kama nukta za nuru angani na ziko mbali sana na Jua na Dunia, na pia Sayari hujongea angani toka sehemu moja hadi nyingine.

Sayari hulizunguka Jua kupitia kwenye njia   maalumu inayoitwa  Obiti au njia ya mzingo.

Hadi sasa Sayari zinazofahamika ni nane tu, nazo ni Zuhura,Zebaki, Dunia, Mirihi,Sumbula,Sarateni, Zohali,na Kausi

Imeandikwa na Eliatosha Maleko (Mwalimu wa Sayansi shule ya Msingi Ilboru)

This slideshow requires JavaScript.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s