Dunia Kupigwa Picha Kutoka Sayari ya Saturn

Ijumaa ya terehe 19 mwezi wa saba mwaka huu, Dunia itakuwa inakiangalia chombo cha Cassini kikipiga picha Dunia kutoka katika upande wa mbali wa sayari ya Saturn. Ambapo mwanga mkali wa Jua utakuwa umekingwa na sayari ya Saturn yenyewe na kufanya ionekane kubwa sana katika sehemu ya mbele ya picha huku sayari yetu ya Dunia ikionekana kama “kiduara kidogo chenye rangi ya blu” kililchopo mbali sana.

SaturnEarthSimulation

Tukio kama hili limeshawahi kutokea katika miaka tisa ya chombo hiki cha Cassin kuzunguka sayari hii yenye pete, lakini wakati huu tukio hili ni la kipekee kabisa. Kwa sababu safari hii wakazi wa sayari ya Dunia watajua mapema kuwa chombo hiki kitapiga picha sayari ya Dunia kutoka katika umbali wa mabilioni ya kilometa.

dayearthsmiled_logo_8.5x11_whtbkg_300dpi_final3Itakuwa ni siku ya Dunia kushangilia, “anasema mkuu wa timu ya kupiga picha Carolyn Porco wa Space Science Institute iliyopo Boulder, Colorado ambaye aligundua uwezekano huu wa kipekee wa kupiga picha hii.

Wanaastronomia Wasiokuwa na Mipaka wanayofuraha kuandaa tukio kubwa la kiastronomia Duniani wakiadhimisha siku Dunia Iliyotabasamu wakishirikiana na muasisi Carolyn Porco.

Sheherekea kwa Kuandaa Tukio, Kuhudhuria Tukio au Shiriki katika Shindano. Na hivi ndivyo unavyoweza kufanya:

awb_fc_300x82Shiriki katika shindano moja au yote Mawili yanayoendeshwa na Diamond Sky Productions:

 • Wasilisha picha inayowakilisha sayari ya Dunia. Picha itakayoshinda itajumuishwa katika ujube utaorushwa katika Milky Way kwa kutumia large radio telescopes.
 • Je wewe ni mtunzi? Tengeneza an uplifting composition kutengeneza siku Dunia iliyotabasamu
Advertisements

2 thoughts on “Dunia Kupigwa Picha Kutoka Sayari ya Saturn

 1. Jose says:

  Wakubwa. Nasikia eti Dunia inaelea angani.
  na kingine eti tunaoishi ndani ya Dunia, tupo kama vile ndani ya Yai ,,,,!!!
  alafu kuna hao wenzetu wa Marekani wanaenda sayari ya Jirani wanapitia wapi,,??
  na wakati tupo ndani ya Yai!!!!

  • unawetanzania says:

   Ni kweli kuwa Dunia haijashikiliwa na kitu chochote zaidi ya nguvu ya uvutano kati yake na magimba mengine yaliyopo angani. Pia si kweli kuwa sisi tunaishi ndani ya Dunia, bali tunaishi juu ya uso wa wa Dunia. Nikitumia mfano wako wa yai, maana yake ni kuwa tupo juu ya hilo yao. Hivyo kutoka kwenda sayari ya njiani ni rahisi sana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s