Naiona Nuru Yako

NGC_6240Ulimwengu ni mkubwa mno na una sehemu nyingi zilizo wazi. Mwanga kutoka katika nyota ya iliyopo karibu zaidi na nje ya mfumo wetu wa Jua unasafiri katika sehemu iliyowazi na yenye giza kwa miaka 4.2 kabla ya kufikia macho yetu, ingawa mwanga ndio kitu kiendacho kwa kasi kabisa kuliko kitu kingine chochote kile katika Ulimwengu, na sisi tunaishi katika sehemu yenye msongamano mkubwa ya anga! Pamoja na anga kuwa na sehemu hizi za wazi kugongana kwa galaksi ni kitu cha kawaida kuonekana. Moja kati ya migongano hiyo ni huu uliochukuliwa katika picha hii, ambayo inaonyesha gimba kubwa la gesi zenye kuwaka linalozunguka galaksi zilizogongana liitwalo NGC 6240.

Galaksi hizi mbili kubwa zinazoonekana katika picha hii zinafanana kwa umbo na ukubwa kama galaksi yetu ya Milky Way. Galaksi zote mbili zinaamiika kuwa na mashimo meusi makubwa katika viini vyao, ambayo yanazungukana na kukaribiana hata muda huu tunapoongea. Inaelekea muda si mrefu yataungana pamoja na kutengeneza shimo kubwa zaidi jeusi!

Athari nyingine ya mkusanyiko huu ni kuzaliwa kwa mamilioni ya nyota mpya katika mchanuo wa nyota angani, ambao umekuwapo kwa muda wa miaka milioni 200! Ulisababishwa na mgongano mkubwa sana ambao ulizikoroga gesi katika galaksi hizi. Mchanuo huo wa nyota ulisababisha kuzaliwa kwa nyota nyingi zenye nguvu zaidi ya Jua, ambazo zilifika tamati ya miasha yao kwa milipuko mikubwa ya supanova na kupelekea maada katika magimba makubwa ya gesi yanayozizunguka galaksi hizi, na kutengeneza nuru ya gesi zinazowaka, ambayo ina maada za kutosha kutengeneza majua bilioni 10!

Dokezo

Je nini kitaitokea kwa NGC 6240  huko mbele? Katika makadirio yote inaonyesha kuwa galaksi hizi mbili zenye umbo la sahani zinaungana na kutengeneza galaksi kubwa lenye umbo la yai. Galaksi za aina hii huonekana za duara, zisizokuwa na umbo maalum, kama vile mikono ya galaksi yetu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s