Kuzaliwa katika Mazingira Magumu

Katika Milky Way – galaksi ambayo tunaishi ndani yake nyota huzaliwa katika nyumba salama, iliyozungukwa na wingu la gesi laini na lisilotembea. Lakini kuna utofauti gani kwa galaksi ndogo iliyopo katika umbali wa miaka ya nuru milioni 55! Galaksi hii kibete ambayo kwa sasa inapita katika kundi la galaksi  katika mwendo wa kujikongoja Kilometa 1000 kwa sekunde, huacha mkia mrefu wa gesi. Tofauti na ndani ya Milky Way yetu, hali katika mkia huu ndio kitu unachoweza kusema ni cha kipekee. Jotoridi huwa kali na kufikia hadi nyuzi joto milioni moja na upepo mkali wa kimbunga unaopuliza katika spidi ya ajabu ya kilometa 4 kwa saa.

fig1Wanaastronomia wa kijapani wamegundua kuwa, nje ya kuwa na matukio ya ajabu, nyota pia zimefanikiwa kuzaliwa katika mkia huo. Mfumo wa namna hii wa kutengenezwa kwa nyota haujawahi kuonekana katika Milky Way. Lakini cha kushangaza ni kwa baadhi ya nyota kuweza kujitengeneza katika mazingira hayo magumu. Kwa nyota zilizopo katika mazingira salama ya Milky Way, hii inaweza kuonekana kama kuzaliwa katika rollercoaster itembeayo kwenye tanuri (oven), mazingira yasiyowezekana kabisa kwa kitu kuzaliwa.

Wakati wa kuangalia kwa ukaribu katika moja ya nyota hizi jasiri ndani ya mkia wa nyota, wajapani hawa waligundua kitu kingine cha kushangaza: ilikuwa inatupa gesi katika spidi ya kilometa 160 kwa sekunde. Nyota hizi zilizo nje ya galaksi yetu ni sawa na wanyama wa porini! Tukizilinganisha, Jua letu linaonekana laini mno!

Dokezo 

Galaksi kibete hii inakatiza katika kundi liitwalo Virgo cluster. Cluster ni kundi la galaksi zenye uhusiano wa karibu. Galaksi yetu ya Milky Way ni sehemu ya cluster nyingine iitwayo Local Group.

Bofya hapa kupata nakala nzuri ya kuchapisha
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s