Kuna Kitu Hakiko Sawa Hapa

Wanaastronomia ni watu muhimu sana katika kufichua siri za anga, na sio kupiga picha nzuri za  kupendeza tu, ingawa tunazipenda pia. Picha hii nzuri ya kupendeza iitwayo ‘Lobster Nebula’ ilipigwa katika uchunguzi unaoendelea kwa kutumia telescope iitwayo VISTA. Uchunguzi huu utachora ramani ya umbo la galaxy yetu ya ‘Milky Way’, na kutusaidi kufahamu ilitengenezwaje.

Picha hii inaonyesha sehemu ya anga iliyozingirwa na wingu kubwa la gesi na kuacha michirizi ya giza na vumbi iitwayo Nebula. Mawingu haya yana nyota changa zinazokuwa ndani yake na zinazowaka katika mwanga wa blue na mweupe wakati zikiangaliwa katika mwanga uonekanao kwa macho. Ingawa VISTA inaangalia anga katika miale ya infra red, miale ya mwanga ambao macho yetu hayawezi kuitambua. Picha hii inaonekana tofauti kabisa ikiangaliwa katika mwanga wa kawaida ambao macho yanaweza kuuona. Iangalie hapa, na uweza kuelewa ni kwanini wingu hili pia huitwa Lobster Nebula au Nebula ya Kaa.

Mwanga unaoonekana unang’aa karibu na katikati ya picha unaitwa ‘Pismis 24-1’. Kwa mda mrefu wanaastronomia wamekuwa wakiamini kuwa hii ni nyota kubwa kabisa katika anga zima, ikiwa na maada mara 300 zaidi ya Jua. Lakini walikuja kugundua kuwa haiko peke yake, na kuwa kuna nyota tatu kubwa zenye kung’aa sana hapo hapo! Hata hivyo, nyota zote hizi tatu ni kati ya nyota kubwa katika galaxi yetu.

Dokezo: Baadhi ya wanasayansi wanafikiri kuwa kwa kila nyota 2 kati ya 3 zipo katika makundi ya nyota kama Pismis 24-1. Lakini ni vigumu sana kuwa na uhakika kwani kuzitenganisha nyota ambazo zipo karibu karibu sana ni kazi ngumu mno. Lakini nje ya mfumo wa nyota karibu na Jua, karibu nusu ya nyota zinajulikana kuwa zipo katika makundi ya nyota!

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s