Kuwasha Moto Anga la Usiku

Jua humulika anga wakati wa mchana, na sehemu za anga zenye mwanga na zinazomeremeta katika anga la usiku ni nyota — maburungutu makubwa ya gesi zinazowaka. Nyota zinazaliwa chini kabisa ya mawingu mazito ya gesi katika anga. Wanaastronomia wanatuambia hivyo, lakini ili kuweza kuthibitisha hili walihitaji kutengeneza telescope maalum yenye uwezo wa kuchukua mwanga ambao macho yetu hayawezi kuuona. Telescope hizi ziliwafanya waweze kuchungulia katika giza, mawingu ya kutengeneza nyota ili kuweza kutambua kilichojificha humo.

Picha hii ilipigwa na moja ya telescope hizo, iitwayo APEX. Telescope hii yenye nguvu ilibuniwa ili kuweza kutambua joto lenye kutoa mwanga kutoka katika mavumbi, ili kuweza kufichua sehemu zilizojificha ambamo nyota hutengenezwa. Ingawa hatuwezi kuziona nyota zenyewe, joto lake jingi limesababisha mawingu ya jirani kupashwa joto. Sehemu hizi zenye mawingu yaliyo pashwa joto zimeweza kupigwa picha na APEX. Katika picha zinaonekana katika rangi ya chungwa ya kupendeza. Je haionekani kama vile nyota changa imewshasha moto mawingu?

DOKEZO: Kukusanya mwanga usioonekana (mwanga ambao macho yetu hayawezi kuuona) ni jambo gumu sana. Kama telescope yako ipo ardhini, basi taarifa kutoka angani zitajichanganya na taarifa kutoka katika tabaka letu la hewa. Ili kuzuia, wanaastronomia wametuma maputo juu angani yakiwa na vifaa ndani yake ili kulisoma anga. Moja kati ya maputo haya yamefika umbali wa Kilometa 50 juu! 

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s