Utafutaji wa Chanzo cha Ulimwengu Umeanza

Leo hii telescope mpya iitwayo ALMA imefungua macho yake. Telescope hii ni kubwa kuliko zote hapa Duniani; imetengenezwa na antenna 54 za madishi yenye mita 12 (sawa sawa na jengo lenye ghorofa nne!) na pia antenna ndogo kumi na mbili zenye mita 7. Madishi haya 66 yatakuwa yanafanya kazi kwa pamoja ili kufanya telescope yenye nguvu katika uso wa Dunia! ALMA inaweza kuona mwanga kutoka katika vitu vilivyo mbali sana katika ulimwengu, ili kutuonyesha taarifa ambazo hazijawahi kuonekana za mwanzo wa ulimwengu. Picha hii ya kupendeza inaonyesha Telescope ya ALMA ilivyotapakaa kukatiza jangwa la Atacama nchini Chile.

Wakati Ulimwengu ulipokuwa mchanga, ulikuwa umejawa na ukungu mzito wa gesi ya haidrojeni. Hii ilifanya iwe ngumu kuuchunguza kwa kutumia telescope zinazotumia mwanga wa kawaida unaonekanao kwa macho. Lakini ALMA ina jicho la pekee ambalo linaweza kuangalia ulimwengu katika mwanga tofauti ujulikanao kama ‘mwanga wa radio’. Hii itaifanya telescope hii iweze kupenya katika ukungu na kuonyesha siri zilizijificha humo kwa mara ya kwanza.

ALMA pia inaweza kutupa ufahamu wa vitu vyenye ubaridi sana katika ulimwengu. Itaweza kupenya katika magimba meusi ya gesi na vumbi ambayo yana jotoridi lililopo chini kidogo ya absolute sifuri — ambao ni ubaridi wa chini kabisi unaoweza kufikiwa (-273 °C). Ubaridi unaoweza kukaribia ubaridi wa kutembea kusini na kuelekea kizio cha kusini cha Dunia! Tunategemea kuvumbua sayari mpya ambazo zinazunguka majua mengine ya mbali na nyota mpya zinazozaliwa katika magimba manene.

Kama unataka kuwa wa kwanza kujua siri zinazovumbuliwa na ALMA kuhusiana na chanzo cha ulimwengu wetu, basi hakikisha unasoma space scoops katika miezi inayofuta!

Dokezo: ALMA imetengenezwa katika mlima wenye mwinuko wa mita 5000 uliopo katika jangwa la Atacama, Chile. Moja kati ya sehemu kame zaidi katika Dunia! Mwinuko huu mkubwa na ukame uliopo katika eneo hilo unamaanisha kuwa kuna kiasi kidogo sana cha mawingu kinachoweza kuingilia uchunguzi. Lakini katika mita 5000 hewa ni ndogo sana, hivyo binadamu hawakai sana katika eneo hilo.

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari vya ESO naNAOJ

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s