Nyota Kupe!

Wanaastronomia wamepiga picha nzuri sana ya nyota ambayo imepoteza maada zake kutokana na nyota kupe!

Picha hii inaonyesha sehemu ambapo nyota kubwa (ina rangi nyekundu) na nyota kupe (yenye rangi ya blu) katika picha zilizopigwa katika tofauti ya mwezi mmoja na nusu, huku zikizungukana.

Viini vya nyota hizi mbili vinatenganishwa na umbali uliozidi kidogo sana wa ule uliopo kati ya Jua na Dunia. (Kwa kulinganisha, Jua na nyota yake ya karibu vinatenganishwa na umbali wa mara 870,000 ya umbali huu!). Kwa sababu nyota hizi zipo karibu karibu sana, nyota kupe imeshakula karibu nusu ya ujazo wa nyota kubwa.

Nyota Kupe!“Tulijua kuwa nyota pacha hizi si za kawaida, na maada zinahama kutoka katika nyota moja kwenda nyingine,” anasema mwanaastronomia Henri Boffin. Lakini jinsi jambo hili linavyofanyika ni tofauti na vile wanaastronomia walivyokuwa wakitarajia.

Uvumbuzi mpya unaonyesha kuwa nyota kubwa ni ndogo kidogo ukilinganisha na wanaastronomia walivyofikiria hapo mwanzo. Hii inamaanisha kuwa haina ukubwa wa kutosha kujaza nafasi kati ya nyota mbili. Kwa ujumla, ina upana mkubwa wa kujaza robo ya umbali huu. Hii inafanya iwe vigumu kuelezea ni kwa jinsi gani maada zinapotea kuelekea katika nyota ndogo, kwani nyota kupe haiwezi kuifikia.

Wanaastronomia wanafikiri kuwa, kuliko kung’atwa na kupe, nyota kubwa imeamua kujitolea kutoa baadhi ya maada zake. Hivyo ile nyota ndogo hula kitu chochote kinachoingia katika njia yake kama kupe rafiki.

Dokezo: Baadhi ya nyota pacha humaliza mzunguko mmoja kuzungukana chini ya masaa 24, wakati nyingine huchukua maelfu ya miaka!

Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari vya ESO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s