Kutoka Mtu Mdogo wa Kijani hadi Galaxi Kubwa ya Kijani!

Kuna watu bilioni saba wengine wanaoishi katika sayari hii pamoja na wewe, watu wenye umri, ukubwa na rangi za ngozi tofauti tofauti. Ingawa kuna karibu ya mara mamilioni ya galaxy katika ulimwengu zaidi ya binadamu! Nazo pia zipo katika namna tofauti tofauti.

Hivi karibuni aina mpya ya galaxi imeongezwa katika orodha. Aina hii mpya ni kubwa na inang’aa kuliko kitu kingine chochote angani, na kama hiyo haitoshi, basi pia zinawaka katika mwanga wa kijani! Hii imewafanya wanaastronomia wazipe jina la ‘green bean’(harage la kijani) galaxy (angalia green bean ndogo ndogo katika picha iliyopigwa angani).

Kutoka Mtu Mdogo wa Kijani hadi Galaxi Kubwa ya KijaniGalaxi hizi mpya ni baadhi ya vitu adimu sana katika ulimwengu kwa ujumla. Tunafikiri kuwa  zinang’aa sana kwa sababu ya shimo jeusi katika viini vyake. Shimo jeusi ni kitu kidogo sana ambacho kina nguvu kubwa ya uvutano. Ambapo kitu chochote kinachosogea karibu na shimo jeusi kinavutwa ndani ya shimo hilo na kutokuonekana tena. Karibu kila galaxy ina kitu kama hicho cha ajabu katika kiini chake, ikiwemo galaxi yetu ya Milk Way!

Kama vile shimo jeusi linavyomeza vitu vilivyo karibu yake na vile vinavyolizunguka. Fikiria kama vile maji yanavyofonzwa katika sinki. Mduara unaozunguka shimo jeusi huongezeka joto kwa kadri jinsi unavyozungushwa na kufanya utoe mwanga mkubwa sana unaong’aa. Kwa kutumia njia hiyo mashimo meusi yanajulikana kwa kutengeneza mwanga mkali kabisa katika viini vya galaxy. Lakini katika green beans, galaxi yote inawaka!

Dokezo: Pamoja na green beans (maharage ya kijani), kuna galaxi za ‘green pea’ (njegere) pia huko angani. Zilizopewa jina hilo kwa sababu zinafanana na njegere (angalia hapa). Galaxi hizi ni ndogo kuliko zile za green bean na zinatoa mwanga mkali sana wa kijani unaotoka kwenye nyota zilizopo ndani yake!

Kwa Taarifa Zaidi

Taarifa hii ya Swahili Space Scoop imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s