Volkano ya Zuhura

Katika Dunia, uji uji unaowaka na kuchuruzika kutoka katika milipuko ya volkano ni moja kati ya mambo makubwa yenye nguvu na kustaajabika ya kiasili. Na sasa wanaastronomia wameweza kugundua kwamba milipuko ya volkano inatokea kwa kasi hata kwenye Zuhura (Venus), sayari iliyo karibu kabisa na Dunia.

Volkano ya ZuhuraKatika mwaka 2005, wanaastronomia walituma chombo kilichoitwa Venus Express ili kuichunguza sayari ya Zuhura kwa ukaribu. Chombo hicho kimekuwa kikizunguka katika obiti ya Zuhura tangu wakati huo. Kwa bahati mbaya hali ya hewa kwenye Zuhura ni ya mawingu  karibu mda wote na kuifanya sayari hii ifunikwe na mawingu, na kukifanya chombo kisiweze kuangalia moja kwa moja volkano zilizopo katika uso wa Zuhura. Hivyo wanaastronomia wakaamua kutumia ujanja; na kutafuta gesi maalum ambayo huwa inatolewa pale volkano inapokuwa imelipuka. Gesi hii kuna wakati ambapo huwa inaonekana katika wingu zito la Zuhura na kufanya Venus Express iweze kuiona. Kwa kutumia chombo hicho, waliweza kuona mabadiliko makubwa ya kiwango cha gesi katika mawingu. Hivyo kuwafanya wafikilie kuwa gesi hizi zinatoka katika milipuko ya volkano.

Katika kipindi cha nyuma, Venus express pia iliweza kupata dodoso za kuwepo kwa volkano. Kwa kutumia kamera maalum inayoweza kuona katika mawingu na kuangalia tofauti ya jotoridi. Kwa kutumia kamera hii ileweza kugundua kitu kilichoonekana kama uji uji wa volkano unaotembea. Hii inaonyesha kuwa jirani yetu sio tu ana hali ya hewa mbaya yenye dhoruba nyingi na joto kali bali pia ardhi yenye inatokota.

Dokezo: Zuhura ni moja kati ya vitu vinavyong’aa sana angani. Lakini huwa inaonekana katika mda fulani tu na kwa kipindi kifupi; kabla ya mawio (angalia upande wa mashariki) au kabla ya machweo (angalia upande wa magharibi).

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s