Kutoka Nafaka hadi Kikombe Kitakatifu

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukifahamu kuwa sayari hutengenezwa na kuishi kando kando ya nyota. Kwa mfano, Jua ni nyota mzazi wa sayari zote zilizopo katika mfumo wa Jua. Ingawa kwa sasa wanaastronomia wamegundua kuwa kuna aina nyingine ya vitu vyenye uwezo wa kutengeneza sayari zao zenyewe pia! Hii inamaanisha kuwa, sayari zinazofanana na Dunia zinaweza kuwa ni nyingi mno ulimwenguni kuliko tulivyodhania hapo awali! 

Nyota inapozaliwa, mabaki ya gesi na vumbi hutengeneza kisahani (pete) kuizunguka, mfano ni pete zinazo izunguka sayari ya Satani. Kuna wakati ndani ya visahani hivi, punje ndogo mfano wa nafaka zilizotengenezwa na miamba hujitengeneza. Punje hizi huweza kugongana na kunatana na kutengeneza kitu kikubwa zaidi na kupelekea kuzaliwa kwa sayari.(Angalia video hii ya kupendeza ili kuona ni vipi haswa inatokea!)

Kutoka Nafaka hadi Kikombe KitakatifuKwa mara ya kwanza kabisa wanaastronomia wamegundua punje ngumu katika kisahani kilichozungukwa na gesi na kuizunguka nyota iliyodumaa “Brown dwarf” — ambayo sio nyota wala sayari.  Brown dwarf pia hujulikana kama nyota iliyoshindwa kuzaliwa. Kwa ujumla ni kubwa sana kuwa sayari, na kuna wakati inakuwa na ukubwa mara 80 zaidi ya sayari ya Jupita ambayo ni sayari kubwa kabisa katika mfumo wetu wa Jua, ambayo pia ni ndogo sana hadi kuwa na uwezo wa kuchoma mafuta katika kiini chake ili kuweza kuwaka kama nyota.

Wanaastronomia hawakutegemea kugundua punje hizi ngumu karibu na brown dwarfs kutokana na sababu mbali mbali, kwanza visahani vinavyozunguka brown dwarfs hizi havina maada nyingi, hivyo uwezekano na chembe chembe kugongana na kutengeneza tufe kubwa ni mdogo sana. Ijapokuwa inaonyesha kuwa mawazo yao hayakuwa sahihi kwani chembe chembe hizo zinapatikana katika visahani vya brown dwarfs. Pia inawezekana kuwa chembe chembe hizi ndogo zimeshajikusanya katika miamba minene inayolingana na sayari, na kutoa uwezekano mkubwa wa kugundua sayari yenye ukubwa kama wa Dunia huko angani!

Dokezo: Brown Dwarfs haziwezi kung’aa kama nyota, ingawa zinamng’ao. Hii inatokana na nguvu ya uvutano inayogandamiza na kusukuma maada katika kiini chake. Hivyo kuifanya brown dwarf kutoa mwanga mwekundu hafifu wenye kung’aa.

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s