Anga Inaweza Kulipuka!

Mashimo meusi yana sifa mbaya kutokana na sifa yake ya kumeza kila kitu ndani yake na kuvipoteza moja kwa moja. Sifa nyingine ambayo haijulikani sana ni kwamba yana uwezo wa kutengeneza milipuko na kutupa vitu kwa nje. Wanaastronomia wameweza kugundua milipuko ya aina hii miwili ambayo yote imeweza kuvunja rekodi!

Galaxi nyingi zina mashimo meusi katika viini vyake, ikiwemo galaxi yetu ya Milk Way. Mashimo haya meusi yanaweza kuwa na uzito zaidi ya mara millioni ya ule wa Jua letu, ambao umekandamizwa katika duara dogo. Maada zilizopakiwa katika duara hilo huwa na nguvu kubwa sana ya mvutano, na kuweza kumeza hata mwanga!

Anga Inaweza KulipukaMashimo meusi yanajulikana sana kwa uwezo wake wa kuvuta maada ndani, kama vile maji yanavyoweza kumezwa katika shimo la sinki. Maada hizo hutengeneza umbo la kisahani kulizunguka shimo jeusi kwa kadri linavyozidi kumeza maada. Milipuko hii mara nyingi huonekana kutokea katika viini vya galaxi zinazowaka sana viitwavyo ‘quasars’.

Mmoja kati ya milipuko iliyogunduliwa upo mbali sana tena ni karibu kabisa katika na ukingo wa ulimwengu tunaoujua! Wakati mlipuko ule mwingine unaweza kutoka maada ambazo ni sawa na majua 400 kila mwaka! na nishati ya karibu mara 100 ya nishati ya nyota zote zinazopatikana kwenye Milk Way galaxi. Hii si nguvu ya kawaida!

Dokezo:Mashimo meusi sio mashimo kama unvyoweza kudhania na ni kinyume cha kitu kuwa kitupu. Kwani mashimo haya yamebeba maada nyingi ndani yake katika eneo dogo la anga huko ulimwenguni. Jaribu kutengeza modeli ya shimo jeusi kwa kutumia muongozo huu wa UNAWE ili kugundua zaidi kuhusiana na mashimo haya ya ajabu.

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hiiimetokana na taarifa kwa vyombo vya habari vya ESO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s