Kupuliza Mapovu

Wanaastronomia wamepiga picha tukio adimu sana huko angani: liitwalo ‘kuzaliwa upya kwa planetary nebula’. Hili ni povu la gesi ndani ya povu la gesi lenye rangi ya kahawia, au nebula, kama unavyoweza kuliona katika picha hii. Nyota nyingi hugeuka nebula mwishoni mwa maisha yake, na wakati mwingine tukio hili hufanyika mara mbili kama ilivyo kwa hili.

Kupuliza MaputoEndapo nyota kama Jua letu inapomaliza mafuta yake yote, hutanuka katika umbo kubwa la red giant ambalo ni kubwa zaidi ya mara kumi ya saizi yake ya awali. Katika hali hiyo nyota huishiwa nguvu za kuweza kushikilia matabaka yake ya nje, ambayo huishia kutawanywa angani. Wakati huo huo mabaki baki ya kiini hushambulia matabaka hayo yaliyolegea kwa mionzi mikali sana kutoka ndani na kuyafanya yabadilike na kuwa planetary nebula – mawingu ya gesi yenye rangi rangi.

Mara chache sana huwa inatokea kiini pia hutanuka na kutengeneza nebula. Na ikitokea hivyo huwa tunasema ni ‘kuzaliwa upya kwa planetary nebula’. Ukilinganisha na maisha ya nyota nebulae (wingi wa neno nebula) huishi kwa mda mfupi sana. Hupotelea huko angani ndani ya miaka elfu tu! Hii husababisha ugumu katika kuziona nebulae na haswa zile zilizozaliwa upya. Lakini kwa wakati huu wanaastronomia wameweza kuipiga picha moja wapo.

Dokezo: Katika karne zilizopita, watu walikuwa wanafikiri wanaangalia sayari iliyozungukwa na gesi pale walipoona rangi rangi za planetary nebula kwa kutumia telescope na kusabisha kupewa jina hilo.

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya NASA Chandra X-ray Observatory Press Release.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s