Nyota Zilizostaafu na Kinyago!

Mara nyingi watu wakistaafu huchukucha fani mpya ili kufidia mda wao, kama vile kuchora au kuvua samaki. Wanaastronomia katika siku za karibuni wameziona nyota mbili zilizostaafu ( ziitwazo mbilikimo weupe), katika kiini cha nebula ya kupendeza iliyochukua sura ya kinyago! Maada za rangi nyekundu zinachochirizika kutoka katika kila kona ya nebula hii zimejikunja katika mfumo wa S baina ya nyota hizi mbili za zamani.

Nyota kama Jua ikiishiwa nishati, inaanza kubomoka ndani kwa ndani. Maada zilizopo katika kiini chake huishia kugandamizwa katika tone dogo lenye uzito mkubwa. Tone hili dogo huitwa mbilikimo mweupe. Nyota hiyo pia hupoteza gamba lake la nje la gesi,na kuelea angani. Gesi ambazo hutengeneza planetari nebula – ambayo ni mawingu ya kupendeza yanayozunguka mbilikimo mweupe, kama yalivyoonyeshwa katika picha.

Nyota Zilizostaafu na KinyagoSio jambo lililozoeleka kwa wanaastronomia kuziona nyota mbilikimo nyeupe zikiwa zinazungukana katika mfumo unaoitwa mfumo pacha na wanaastronomia. Pia ni aghalabu sana kwa nyota hizi kuwa karibu karibu sana! Wanaastronomia wanatarajia nyota za mbilikimo weupe kuchukua miongo kadhaa ili kukamilisha mzunguko mmoja kuzungukana, lakini kwa hizi mbili huchukuwa muda wa kama siku moja hivi!

Kadri nyota hizi zinavyozidi kuzungukana, huathiri utupwaji wa maada kutoka katika kiini chake, na kuzisababisha kujipinda katika upo la kuvutia la S.Wanaastronomia wametumia miaka mingi wakistaajabu ni kwa jinsi gani michirizi hii ya kupendeza inavyotengenezwa na sasa wameweza kujua!

Dokezo: Kipande cha mbilikimo mweupe chanye ukubwa na donge la sukari kinaweza kuwa na uzito sawa na kiboko!

Taarifa hii ya Swahili Space Scoop imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO na SAAO

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s