Safari ya Kutembelea Shule ya Nyota

Kama ungetaka kujua kuhusu vijana, basi ungetaka kutembelea katika shule ambapo kuna vijana wengi, au sio? Picha hii inaonyesha shule ya nyota – nyumba ambayo ina maelfu ya nyota kubwa na changa zenye kung’aa sana angani. Kundi la nyota liiltwalo Cygnus OB2 ni moja kati ya sehemu za mwanzo zinazoangaliwa na wanaastronomia wakitaka kuchunguza nyota changa.

Cygnus OB2 ni kundi kubwa la nyota katika nusu ya kipande cha kaskazini cha anga, lina jumla ya maada mara 30,000 zaidi ya Jua! Pia ni kundi lililo karibu kabisa na Dunia yetu. Je ni kwanini hukuwahi kusikia kuhusiana na kundi hili kabla? Hii ni kwa sababu limejificha nyuma ya wingu zito la vumbi. Ili kuweza kulichunguza, wanaastronomia wanahitaji kutumia telescope inayoweza kuona katika miale ya X-ray na infrared. Aina hii ya miale inaweza kupenya katika wingu zito ambapo mwanga wa kawaida hauwezi kupenya.

Safari ya Kutembelea Shule ya NyotaMoja kati ya vumbuzi za kufurahisha na ambazo ni adimu sana zilizowahi kufanywa na wanaastronomia wakati wa kuchunguza nyota kubwa na changa zipatikanazo katika kundi hili ni, nyingi ya nyota zina sayari chache ukilinganisha na nyota nyenzao katika makundi mengine madogo. Na nyingine hazina sayari kabisa!

Wakati nyota inatengenezwa, huwa kuna maada ambazo huachwa. Maada hizi hutengeneza tabaka la vumbi na uchafu, kama tabaka nene la pete ya Satani. Ndani ya tabaka hili punje ndogo ndogo za vumbi zilizotengenezwa na miamba na barafu hutengenezwa, na kuna wakati vipande hivi huungana na kutengeneza mawe makubwa – fikiria kama unatupa jiwe la barafu kwenye theluji, hukuwa kubwa kwa jinsi linavyokusanya theluji. Na hivi ndivyo sayari zinavyotengenezwa katika ulimwengu.

Ijapokuwa nyota changa na nzito pia ina uwezo wa kuharibu vibaya tabaka la vumbi la nyota ya jirani kutokana na nishati nyingi iliyokuwa nayo, kabla sayari yoyote haijatengenezwa katika nyota hiyo! Hii inamaanisha kuwa Cygnus OB2 na nyota nyingine kubwa hazina sayari zozote kama tulivyofikiria hapo mwanzo!

Dokezo: Moja kati ya nyota ang’avu kabisa katika galaxi yetu inaishi katika kundi hili, na ni ang’avu mara milioni mbili ukilinganisha na Jua!

Swahili Space Scoop hii imetokana na NASA Chandra X-ray Observatory

Advertisements

2 thoughts on “Safari ya Kutembelea Shule ya Nyota

 1. otraiespeja.blogs.lv says:

  I’m not sure where you are getting your info,
  but great topic. I needs to spend some

  time learning much more or understanding more.
  Thanks for excellent

  info I was looking for this info for my mission.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s