Kusheherekea Space Scoop ya 100!

Universe Awareness (UNAWE) au Ufahamu Ulimwengu wana furaha kutangaza shehere maalum kwa huduma yake ya habari kwa watoto: Habari ya leo Nyota Nzee Kijana ni ya 100 tangu kuanzishwa kwa Space Scoop!

Timu iliyopo nyuma ya Space Scoop imepata nafasi ya kuakisi na kuzikumbuka habari mbali mbali zilizowahi kutolewa. “Nafikiri habari nnayoipenda zaidi bado ni ile ya Ulimwengu Ulikuwa na Ukungu” anasema Sarah Reed, mwalimu wa sayansi wa EU-UNAWE aliyepita. “Unaweza kuvuta fikra jinsi nilivyo hamaki pale nilipoambiwa niandike habari kuhusiana na dhama za kujichaji upya ‘era of reionisation’ kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 8. Lakini ni ugumu wa mada yenyewe ndio uliofanya kazi hii iwe ngumu kwangu mimi. Ni changamoto yenye kufariji katika kuwasilisha sayansi ya astronomia ambayo ni ngumu kwa watoto bila kujali ugumu wa mada yenyewe inayozungumziwa.”

Tangu ilipozinduliwa space scoop ya kwanza mwezi Februari 2011 kwa ushirikiano na European Southern Observatory, kumekuwa na wadau wengi zaidi waliovutiwa: Netherlands Institute for Radio Astronomy (ASTRON), NASA’s Chandra X-ray ObservatoryDutch Research School for Astronomy (NOVA), Europlanet, the Royal Astronomical Society (RAS), the Southern African Astronomical Observatory (SAAO) na the European Space Agency (ESA).

Familia hii ya Space Scoop inayokua ina ongezeko la idadi za habari zitolewazo, ambapo utathimini wa ndani wa timu umedhamilia kuhakikisha kuwa ubora wa habari hizi haupungui. “ Ni changamoto kubwa kutengeneza Space Scoop ambayo inavutia na yenye kuaelimisha,” anasema Natalie Fischer, kutoka EU-UNAWE Ujerumani, ambae hufanya kazi ya kutathimini ubora wa elimu iliyopo kwenye Space Scoop.” Japokuwa kila wakati ninapojadili habari mpya ya Space Scoop na watoto katika darasa langu na kuona macho yao yakiangaza zaidi kutokana na kuvutiwa na kustaajabu, najua kuwa nimefanya kazi nzuri kwa mara nyingine tena!”

Katika kuadhimisha sherehe hii maalum, EU-UNAWE wametoa dhana za kufundishia za darasani, ziitwazo Space Scoop Storytelling (Simulizi za Space Scoop), ambazo hutumia hadithi za habari kwa kujenga  ubunifu katika kuandika na kuchora. Shughuli hii pia inaanzisha uhandishi wa habari kwa watoto, katika kupanua wigo wao katika tamsinia ya sayansi.

Space Scoop pia ni nyenzo nzuri kwa kufundishia hata nje ya darasa, kama jinsi ilivyoweza kuonyeshwa na Universe Awareness Romania. Timu ambayo ilizindua maonyesho ya Space Scoop mapema wiki hii, yaliyoitwa Space Scoop – What’s New in the Universe? “Space Scoop – Je ni nini kipya huko Ulimwenguni? Maonyesho yanayofanyika katika Maktaba ya Metropolitan iliyopo Bucharest hadi tarehe 9 Novemba 2012.

UNAWE itatoa kitabu cha Space Scoop mapema mwakani. Zaidi ya hapo makala kuhusiana na uzoefu uliopatikana kutokana na kuandika Space Scoop kwa ajili ya watoto wadogo utakuwa ni sehemu ya toleo lijalo la Communicating Astronomy with the Public Journal “Jarida la Uwasilishaji wa Astonomia katka Jamii” litakalo toka mwishoni mwa Novemba.

Maoni Kutoka Katika Jamii ya UNAWE:

Amelia Ortiz-Gil, Hispania

“Sisi [katika Chuo Kikuu cha València] hupokea watembeleaji kutoka katika shule mbali mbali mara tatu kwa wiki. Space Scoop hutuwezesha sisi kuwafahamisha watoto hawa uvumbuzi mbali mbali wa kiastronomia, kuwaambia kuwa bado kuna vitu vingi sana ambavyo hatuvifahamu na kwamba wao wanaweza kuwa kizazi kijacho cha wavumbuzi.”

Mponda Malozo, Tanzania

“Baadhi ya walimu na watoto hawajawahi kuweza kuweka uhusiano kati ya kile wanachofundishwa darasani na kile wanachokiona katika dunia halisi. Space Scoop inatengeneza uhusiano kati ya vitu hivyo viwili, katika lugha rahisi na inayoeleweka”.

Avivah Yamani, Indonesia

“Huwa tunachapisha Space Scoop katika jarida la Astronomi hapa Indonesia ili kutambulisha astronomia kwa watoto, na pia makala katika tovuti yetu. Pia tunatumia makala mbali mbali kwa ajili ya kusimulia hadithi na uwasilishaji katika shughuli zetu na jamii.”

Kwa Taarifa Zaidi:

Space Scoop ni huduma ya kwanza ya habari za kiastronomia kwa ajili ya watoto wa miaka 8 na kuendelea zinazoandaliwa na programu ya Universe Awareness. Wazo lililopo ni kubadilisha jinsi sayansi inavyochukuliwa na watoto wadogo, kana kwamba ni somo lililopitwa na wakati na lenye kufadhaisha. Kwa kuwapa habari za kuvutia za uvumbuzi wa kiastonomia, tunaweza kuwashawishi kupenda sayansi na teknolojia. Space Scoop ni dhana nzuri inayoweza kutumika darasani kufundisha na kujadili habari za astronomia za hivi karibuni.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s