Kuangalia Ndege Angani

Je ushawahi kuangalia angani na kuona maumbo ya kufikirika yanayotengenezwa na mawingu? Wanaastronomia pia hufanya vitu vinavyofanana na hivyo, ijapokuwa mawingu wanayoyatumia wao yanaitwa nebula na yapo katika anga za mbali sana. Mawingu haya yanatofautiana na ale ya duniani kutokana na kutengenezwa na gesi na vumbi za angani, ukilinganisha na yale ya tunayo yaonayo angani yaliyotengenezwa kwa maji. Ambapo wanaanga wameweza kuona umbo linalofanana na kichwa cha ndege katika mzunguko wa wingu uitwao Seagull nebula.

Gesi na mavumbi ya angani ni vya baridi, hivyo having’ai na kutoa mwanga wa kutosha kuweza kuonekana kwa macho yetu, kwani vitu vyenye joto jingi ndivyo vyenye mwanga mwingi. Hali hii huweza kujitokeza katika hali ya kawaida pia, ambapo kama umeshawahi kushika balbu ambayo imewashwa kwa mda mrefu unaweza kuona kuwa ina joto sana! Na nebula katika picha unayoiona ni nyekundu kwa sababu ya nyota yenye joto kali iliyopo kati kati yake, nyota ambayo unaweza kuiona imekaa kama jicho la ndege seagull. Na joto kutoka katika nyota hiyo linafanya gesi zinazoizunguka ziweze kung’aa na kutoa mwanga unaoonekana.

Katika picha pia unaweza kuona ukungu wa rangi ya blu, je umeuona? Ukungu huu ni mavumbi ambayo yameangazwa na joto kutoka katika nyota changa zinazopatikana ndani ya nebula hii. Mwanga wa nyota hizo huakisiwa kutoka katika chembe chembe za mavumbi yapatikanayo angani na hivyo kuzifanya zionekane, kama vile unavyoweza kumulika kitu kwa tochi katika chumba chenye giza: ambapo utaweza kuviona vitu hivyo kwa sababu mwanga kutoka katika tochi yako huakisiwa na kurudi katika macho yako.

Picha hii inaonyesha sehemu ndogo tu ya nebula, ambapo wingu zima limetawanyika kama mabawa ya ndege katika sehemu kubwa ya anga na kufanya ionekane kama ndege anaruka angani! Angalia tena picha hii vizuri hapa 

Dokezo: Nyota inayoonekana katika kati ya picha hii (kwenye jicho la ndege) ipo pamoja na nyota nyingine ambayo ni jirani. Nyota hizi mbili zinazungukana na kufanya ziitwe nyota pacha “binary stars”! 

Kwa Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari ya ESO 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s