Wiki ya Kimataifa ya Anga Tanzania, 2012

Ni sherehe ya kimataifa ya sayansi na teknolojia pamoja na mchango wake katika ubora wa hali ya binadamu. Umoja wa Mataifa ulitangaza kuanzia mwaka 1999 kufanyika kwa sherehe hii ya Wiki ya Anga Duniani inayofanyika kila mwaka kuanzia tarehe 04-10 Oktoba, tarehe ambazo huadhimishwa matukio mawili makubwa ambayo ni:

• Kurushwa kwa satelaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu tarehe 4/10/1957 iliyoitwa Sputnik 1, ambayo ilikuwa chachu ya wanasayansi kuichunguza anga.
• Kusainiwa kwa mkataba wa kanuni za uchunguzi wa anga na matumizi ya amani ya anga yetu tarehe 10/10/1967, ambapo mwezi na vitu vingine vyote vilivyopo angani  ilijumuishwa.

Madhumuni ya wiki ya Anga Duniani
• Kuwaelimisha watu kuhusu faida tuzipatazo kutokana na anga.
• Kuhamasisha matumizi sahihi na endelevu ya anga kwa maendeleo ya kiuchumi
• Kuonyesha ushirikishwaji wa jamii katika shughuli za uchunguzi wa anga
• Kutoa shauku kwa vijana kuhusiana na sayansi
• Kupelekea ushirikiano wa kimataifa kwenye uchunguzi wa anga na elimu

Jinsi ya Kusheherekea Nchini Tanzania.
Ukiwa nchini Tanzania unaweza kusheherekea sherehe hizi wewe na jamii yako inayokuzunguka kwa kufanya shughuli mbali mbali zinazohusu masuala ya anga kama zilivyoainishwa katika picha hii hapa chini.
1. Udadisi wa Anga
Tukio hili litahusisha watu kuitambua anga yao pamoja na vitu vilivyomo humo mfano: Jua, Mwezi, Nyota, Mawingu, Ndege, Sayari, Upinde wa Mvua na Satelaiti na kuvidadisi.
2. Urushaji wa Roketi
Tukio hili litahusisha watu kujua ni kwa namna gani roketi zinaweza kurushwa kwenda angani kwa kuuliza maswali au kusoma kuhusiana na roketi.
3. Matumizi ya Satelaiti
Tukio hili litalenga watu waweze kufahamu satelaiti ni nini, zinafanya kazi vipi na zinamsaidiaje mwanadamu katika shughuli zake za kila siku mfano TEHAMA (Teknolojia Habari na Mawasiliano).
4. Anga na Utamaduni
Tukio hili lina lengo la kuwafanya watu waweze kufahamu ni kwa jinsi gani utamaduni wao una uhusiano na anga mfano kusoma nyakati kwa kutumia Mwezi au Jua, kutambua nyota kulingana na misimu ya mazao ya matukio mbali mbali ya kijamii, matumizi ya upinde wa mvua na imani mbali mbali zinazohusiana na anga.
5. Kutengeneza Roketi za Karatasi
Tukio hili linalenga kuwafanya watu waweze kutengeneza shepu za roketi kwa kutumia karatasi kwa kufuata hatua zilizoweka katika document ya Origami Roketi (bofya neno Origami roketi kupata document ya kutengeza roketi kwa kutumia karatasi).

Kwa kupata taarifa zaidi, kuweka taarifa ya tukio lako kwenye ramani ya dunia na kuona watu sehemu zingine duniani wanashehereka vipi tafadhali tembelea ya word space week.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s