Telescopes to Tanzania Mafunzo kwa Walimu

Telescopes to Tanzania Mafunzo kwa Walimu ni mafunzo ya wiki moja yenye lengo la kuwajengea uwezo walimu wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, juu ya matumizi ya elimu ya astronomia na anga kuwa chachu ya kongeza udadisi wa wanafunzi katika masomo ya sayansi.

Mafunzo haya yatahusisha jumla ya walimu 80 ambao watapitiwa elimu ya astronomia na jinsi ya kuitumia elimu hiyo katika kufundisha masomo ya hesabati, geografia, fizikia, kemia na biolojia. Pia walimu hawa watapatiwa vifaa mbali mbali vya kuwasaidia katika kufundisha masomo hayo kwa kupitia elimu hii na kupewa mbinu za kuwafanya wanafunzi waweze kuelewa masomo mengine ya sayansi kwa urahisi.

This slideshow requires JavaScript.

Mafunzo haya yatafanyika katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha walimu wa sekondari tarehe 19-23 Novemba 2012, ikifuatiwa na walimu wa shule ya msingi tarehe 26-30 Novemba 2012. Walimu hawa watahitajika kujaza fomu na kuzirudisha katika anuani zilizoainishwa kwenye fomu hizo kabla ya tarehe 1 Octoba 2012 ili kuhakikisha ushiriki wao. Ili kupata fomu ya kujisajili bonyeza hapa kwa ajili ya shule za msingi  au hapa kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari kisha chapisha (print) na uirudishe ndani ya wakati.

Mafunzo haya yatatolewa na walimu wenye uzoefu wa masuala ya astronomia na anga kutoka nchini Marekani, Tanzania na Kenya wenye nia na hali ya kuwezesha walimu wa Tanzania ili kuinua masomo ya sayansi nchini.

Mafunzo haya yemefadhiliwa na wadau mbali mbali wa elimu kutoka katika nchi tofauti tofauti Duniani pamoja na yameratibiwa kupitia Astronomers without Borders , Galileo Teacher Training Program, Global Hands on Universe, Universe Awareness for Young Children –Tanzania, ALCon2012 na Mwangaza Teacher’s Training Center in Arusha. 

Kwa Taarifa zaidi Kuhusiana na Telescopes to Tanzania Project Bonyeza hapa 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s