Watafuta Supanova!

Angalia picha hii mpya ya galaxi kutoka angani, ni picha yenye taarifa nyingi zaidi kuliko picha zote zilizowahi kuchukuliwa katika galaxi hii! Katika picha unaweza kuona kama ni sehemu yenye utulivu, ingawa wanaastronomia wameweza kutambua sehemu yenye milipuko mikali ya nyota mbili katika galaxi hii katika miaka 30 iliyopita.

Mlipuko wa nyota kubwa huitwa Supanova (Supernova), ambayo ni moja kati ya matukio yenye kutoa nguvu/nishati nyingi sana ulimwenguni na mwanga mkali sana, ambapo mara nyingi mwanga huo huweza kuuficha mwanga unaotoka kwenye galaxi nzima kabla ya kufifia ndani ya wiki chache au miezi. Katika kipindi hiki kifupi, supanova huweza kutoa nishati kubwa mno zaidi ya ile inayoweza kutolewa na Jua katika maisha yake yote!

Supanova ya kwanza iliyowezwa kuonwa katika galaxi hii iligunduliwa na profesa wa astronomia kwa kutumia telescope kubwa iliyopo katika jangwa nchini Chile katika bara la Amerika ya Kusini. Ingawa katika ufumbuzi wa hivi karibu katika mwaka 2007, uliofanywa na mtu kutoka Afrika ya Kusini aitwaye Berto Monard, ambaye hupendelea kuchunguza milipuko angani kwa kutumia telescope yake. Berto ni mmoja kati ya watafutaji wa Supanova wengi waliopo Duniani ambao hufanya shughuli hiyo kwa kujifurahisha!

Lakini ni kwa vipi unaweza kuitaftuta supanova? Kwa ujumla ni kwa kupiga picha galaxi kwa kutumia telescope na kuzifananisha na picha zilizochukuliwa zamani. Mabadiliko yeyote ya mng’ao katika galaxi yanaweza kumaanisha kuwa kuna mlipuko wa nyota.

Dokezo: Mwaka uliopita, msichana mdogo mwenye umri wa miaka 10 kutoka Canada aitwaye Kathryn Aurora Gray, alifanikiwa kuwa mtu mdogo kuliko wote kugundua supanova! Labda nawe unaweza kuivunja rekodi inayoshikiriwa na Kathryn! Na kama hauna telescope unaweza kuzitafuta kwa kutumia picha za kutoka angani kupitia tovuvi ya: www.zooniverse.org/project/supernovae

Taarifa Zaidi

Swahili Space Scoop hii imetokana na ESO Press Release

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s