Mbio za Nyota Angani

Hakuna kitu chochote angani ambacho kimesimama, nyota nyingi husogea kama wanariadha wa mbio ndefu ambao hawasimami hadi wafikie mstari wa mwisho, vivyo hivyo nyota huwa zimasogea huko angani ijapokuwa zenyewe hutembea maisha yao yote. Ingawa katika siku za hivi karibuni wanaastronomia wameweza kutambua nyota ambayo inafananishwa wa wakimbiaji wa mbio fupi(angalia nyota iliyozungushiwa katika boxi kwenye picha ).

Ili kuweza kufahamu mwendo kasi wa nyota hii wanaastronomia ilibidi watambue umbali iliyotembea tangu ilipoanza kusogea na kwa mda gani ilichukua kufika umbali huo. Wanaastronomia hawa wanafikiri kuwa nyota hii imeanza safari yake kutokea kati kati ya wingu la gesi na vumbu linaloonekana kwa rangi ya zambarau katika picha. Nyota hii ni maalum kwani inazunguka kwa haraka sana na kutokana na hivyo imejumuishwa katika kundi la nyota zijulikanalo kama pulsar. Pulsar hii ilijietenga na wingu la zambarau wakati wa mlipuko uliotengeneza wingu la gesi na vumbi.
Tathimini ya wanaastronomia imeonyesha kuwa pulsar hii inasogea katika mwendo kasi wa ajabu sana kati ya kilometa millioni 9 na 11 katika lisaa limoja! Mwendo kasi huu unaweza kuifanya nyota hii kuwa na mwendo kasi kupita pulsar zote zinazojulikana hadi leo! Ingawa bado kuna utata katika kupata cheo hicho kwani kuna pulsar nyingine ambayo imekadiliwa kuna na mwendo kasi kati ya kilometa millioni 5 na 10 lisaa limoja.
Ni jambo la kusikitisha kuwa wanaastronomia hawawezi kuzifanya nyota hizi mbili zishindane kukimbia ili kutambua ni ipi ina kasi zaidi ya mwenzake na badala yake inawabidi kukokotoa kwa umakini mahesabu yao ili kujua ipi ina mbio zaidi.
Dokezo: Kama pulsar inasogea katika mwendo kasi wa kilometa 11 kwa saa, hii inamaanisha kuwa inaweza kusafiri kuzunguka mastari wa Equator wa sayari ya Dunia katika sekunde 13!

Taarifa hii ya Swahili Space Scoop imetokana na Chandra X-ray Observatory Press Release

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s