Watanzania,Wanasayansi na Mpito wa Zuhura Kwenye Uso wa Jua

Watanzania kwa mara ya kwanza kabisa wanapata nafasi ya kuzungumza na kudadi kuhusu sayansi ya anga kutokana na tukio adimu kabisa la kukatiza kwa sayari ya Zuhura katika uso wa Jua. Tukio hili adimu kabisa katika maisha ya mwanadamu aliyepo hai leo litashuhudiwa nchini Tanzania wakati wa Mawio (Kuchomoza kwa Jua) kati ya saa 6: 34 am na 7: 49 am (asubuhi) ya tarehe 6 Juni 2012 ambapo watanzania wataweza kuona mwisho wa tukio hili, ambazo sayari ya Zuhura itakuwa inaliacha Jua.

Katika uso wa Jua sayari ya Zuhura itaonekana kama tone jeusi linalotembea kadri mda unavyokwenda. Ili kuweza kuona sayari hii hauna budi kutumia kioo chenye rangi ili kuzuia miale mikali ya Jua inayoweza kudhuru macho yako.

Tukio hili limepata umaarufu mkubwa sana Dunia kutokana na mchango wake katika sayansi, ambapo katika mwaka 1639 mwanasayansi shupavu aitwaye Jeremiah Horrocks aliweza kukokotoa umbali uliopo kati ya Jua na Dunia Kupita tukio hili. Baada ya hapo wanasayansi wengine maarufu kama Sir Isaac Newton na Kepler walipata shauku ya kujua zaidi na kuweza kuja na kanuni mbali mbali za sayansi kama ile ya Nguvu ya Uvutano (Graviational force) na Kanuni za Kepler’s (Kepler’s Laws).

Ingawa Jeremiah Horrock alifariki katika ajali mbaya akiwa na umri wa miaka 22, aliweza pia kukokotoa njia za sayari (obiti) akiwa na umri wa miaka 17 tu! na kufanikiwa kuacha mchango mkubwa katika sayansi ya leo.

Umbali kati ya Dunia na Jua wa Kilometa Millioni 96 uliokokotelewa na Jeremiah uligundulika kuwa sio sahihi na kupelekea mwanasayansi maarufu wa Uingereza, aitwaye Halley kuzitaka nchi zote Duniani ziwatume wanasayansi wake wa anga kwenda kuangalia mpito wa sayari ya Zuhura katika uso wa Jua mwaka 1678.

Wanaanga wa enzi hizo walijua kuwa mikatizo inayofuata ya sayari ya Zuhura itatokea katika miaka ya 1761, 1769, 1874, 1882, 2004 na pia 2012, ambapo nchi kubwa kama Uingereza, Ufaransa, Marekani na Urusi zilijikita katika kuwatuma wanaanga wake.

Wanaanga hawa walitumwa kwenda katika nchi mbali mbali kutokana na kutokuwepo kwa teknolojia za kufahamu mahali pa uonekano wake kwa uhakika. Wanasayansi hawa walikumbana na matatizo mbali mbali njiani na kupelekea nyingi ya safari hizo kutokuwa za mafanikio. Kwa mfano waingereza Mason na Dixon wilisafiri kwa jahazi hadi katika kisiwa cha Sumatra mwaka 1761 ambapo walikuta waingereza wenzao 11 wameuwawa na wafaransa na pia kisiwa cha Sumatra kilikuwa kimeshamilikiwa na wafaransa.

Ingawa hadithi ya kusisimua zaidi ni ile ya wanasayansi wa Kifaransa aliyeitwa Guillame Joseph Hyacinth Jean-Baptiste Le Gentil de la Galaisiere. Yeye alisafiri na meli hadi India ili kuangalia kukatiza kwa Zuhura mwaka 1761. Ila kabla ya kufika, India ilikuwa imeshamilikiwa na waingereza, hivyo kumfanya awe baharini ndani ya meli yake wakati wa tukio na kushindwa kuchunguza chochote labda kutokana na kucheza cheza kwa meli kulikotokana mawimbi ya bahari. Ila mwanasayansi huyu alikuwa shujaa na mwenye shauku, hivyo aliamua kubaki katika bahari ya Hindi hadi pale tukio linalofuta la mwaka 1769 litakapofika.

Katika kipindi cha kusuburi aliweza kutembelea visiwa mbali mbali vya bahari ya Hindi na baadae alielekea Ufilipino ambapo alikuta wahispania wanatawala wakati huo, ambao walimfukuza na akaamua kuelekea Pondicherry (Mji uliokuwa chini ya Ufaransa nchini India).

Alifika kafika katika mji huo kwa wakati kabla ya tukio na alitengeza kituo chake cha kuangalia anga, alirekebisha saa yake na kuweka darubini yake (telescope) tayari kwa tukio la kukatiza kwa Zuhura usoni mwa Jua. Ingawa siku ya tukio ilipofika kulikuwa na mawingu hivyo kuharibu tena uchunguzi wake kwa mara ya pili!

Baada ya hapo alimaua kurejea kwao Ufaransa, ikiwa ni baada ya kupoteza miaka 11. Alipofika nchini kwao alikuta ametangazwa kuwa ni mfu, mke wake ameshaolewa na mtu mwingine na ndugu zake wameshagawana mali zake zote. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani ilikuwa ni kazi ngumu sana kuwa mwana sayansi ya anga katika enzi hizo.

Lakini leo hii sayansi ya anga imekuwa ni rahisi kutokana na maendeleo ya teknolojia, ingawa bado tunatumia elimu na maarifa mbali mbali yanayotokana na wanasayansi waliopita. Mfano kizio cha umbali wa vitu vilivyopo angani kijulikanacho kama Astronomical Unit (AU) kinatokana na uvumbuzi wa Jerehimia Harrocks. Ambapo Astronomical Unit moja ni sawa na umbali kati ya Dunia na Jua ambao leo hii unajualikana kuwa ni 153 +/- 1 Milioni Km.

Ni wazi kuwa wengi wetu hatutaweza kuwa na maisha marefu ya kuona tukio linalofuata, hivyo hatuna budi kufanya kumbu kumbu juu ya vile tulivyoshuhudia wakati wa tukio hili kwa ajili ya vizazi vijavyo. Unaweza kufanya hivyo kwa kupitia Gloria Project(bofya maandishi ya blu).

Zaidi ya hapo ni vyema kusoma zaidi kuhusu tukio hili adimu litakalotokea tena mwaka 2117 (baada ya miaka 105) na kuishirikisha jamii yako katika kuelewa umuhimu wake kwa kusoma taarifa zaidi kupitia chapisho la MPITO WA SAYARI YA ZUHURA JUANI, KUANGALIA MODELI YA MPITO WA SAYARI YA ZUHURA JUANI, KUSOMA JARIDA MAALUM LA MPITO WA SAYARI YA ZUHURA JUANI,  Telescopes to Tanzania Observing notes na pia unaweza soma habari hii kwa Kiingereza hapa.

Habari hii imeandikwa na Mponda Malozo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s