Dhana Potofu ya Kiastronomia

Kwa miongo kadhaa wanaanga wamekuwa wakidhania kuwa kiasi cha mwanga tunachokiona kutoka katika galaxi (Mkusanyiko mkubwa wa Nyota) kuwa kinaweza kutumika katika kutambua kiasi cha maada nyota kinachopatikana kwenye galaxi. Ijapokuwa kundi la wanaanga walipojaribu kufanya jaribio la kisayansi juu ya dhana hii, waligundua kuwa ung’aavu wa galaxi si njia sahihi ya kuhesabu nyota.

Kwanza kabisa, wanaangaa hawa waliangalia galaxi mbali mbali ili kutengeneza modeli ya pande tatu (3D), ili kupata ufahamu wa jinsi nyota zinavyosogea. Baadae taarifa ya modeli iliwekwa kwenye komputa yenye nguvu kubwa (super computer), ili kufahamu ni kiasi gani cha maada nyota kinapatikana ndani ya galaxi hizo. Kwa kutumia komputa hizo wanaanga waligundua kuwa baadhi ya galaxi za zamani ulimwenguni zina nyota mara tatu zaidi ya ilivyodhaniwa kwa kutumia mng’ao wa galaxi.

Lakini ni kwanini maada nyota hizo hazing’ai sana? “Galaxi zinaweza kuwa na idadi kubwa ya nyota ndogo ndogo”, amesema mwanaanga Michele Cappellari. Nyota hizo ndogo haziwezi kutoa mwanga mwingi, lakini zikijumuishwa zote kwa pamoja husababisha kuwepo kwa maada nyota nyingi.  Pia alisema kuwa baadhi ya maada nyota hizo zingeweza kutengeneza sayari. (Kama ilivyo kwa sayari zilizopo katika mfumo wetu wa Jua, ambazo zimetengenezwa kutokana na wingu la gesi na vumbi ilililotengeneza Jua.) Pia baadhi ya maada zinaweza kuwa zimejificha katika nyota zilizokufa na kufanya zising’ae.
Michelle amefurahiswa na uvumbuzi huu mpya na alisema “ Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani kuna mambo mengi ya kugundua, juu ya kukua na kubadilika kwa galaxi na ulimwengu wa mwanzo”

Dokezo: Komputa yenye uwezo mkubwa zaidi ina kasi zaidi ya vicheza michezo vya Sony (Sony S PlayStation 3s) 28 000 vikijumuishwa na consoles!

Taarifa Zaidi 

Kwa kiingereza bofya hapa na hapa kwa kiswahili toka katika tovuti ya UNAWE

Taarifa hii imetolewa na ASTRON kwa ajili ya vyombo vya habari.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s