Shuhudia Mpishano Adimu wa Sayari Zing’aazo Angani

Kama umekuwa mdadisi wa mazingira yako haswa anga yetu, bila shaka utakuwa umeona nyota mbili zing’aazo sana upande wa magharibi wakati wa jioni. ingawa hizi si nyota kama tunavyoweza kudhani au kufahamu katika uelewa wa kawaida bali ni sayari ya Zuhura (Venus) na Sambula (Jupiter) ambazo ninang’aa kutokana na kukisi mwanga wa Jua.

Sayari hizi zimekuwa zikisogeleana siku hadi siku na hatimaye zitaweza kupishana kesho tarehe 15 Machi 2012.Tukio hili ni adimu sana kutokea hivyo limesababisha watu mbali mbali Duniani kuweza kufualia mpishano huu siku hadi siku na kuongeza udadisi wa anga na vitu vilivyomo angani kupitia programu iitwayo Conjuction of Glory (Makutano ya Neema).

Ukiwa Tanzania una nafasi kubwa ya kushuhudia mpishano huu kwa macho au kwa darubini na kuweza kuongeza uelewa wako, jamii ya ko na watoto wanaokuzunguka juu ya mizunguko ya sayari, utofauti kati ya sayari na nyota na pia kuzungumza mengi kuhusu anga na sayansi yake.

Tafadhali endelea kusoma zaidi hapo chini kuhusu mkutano huu kutoka kwa Dr. Jiwaji kwa uelewa zaidi (bonyeza hapa kusoma kwa kiingereza).

SAMBULA KUIPITA ZUHURA ANGANI

Dkt. N T. Jiwaji

Sayari mbili zinazong’aa vikali, Zuhura (Venus) na Sambula (Jupiter) zilizokuwa zikionekana angani tangu Novemba mwaka jana, sasa ziko jirani katika anga za Magharibi saa za jioni ya saa moja.  Sayari zote mbili zinang’aa mno ila Zuhura inang’aa zaidi.

Sayari hizo mbili zitaonekana jirani kabisa jioni ya Alhamisi Machi 15.  Sambula, iendayo polepole sana, itaipita Zuhura baada ya Jumamosi Machi 16 ambapo zitakuwa sawia.  Kuwa jirani angani ni muono wetu tu tunavyoziona, lakini Sayari zenyewe zimepishana angani kwa mamilioni ya kilomita.  Baada ya Machi 16 Sambula itaonekana chini ya Zuhura kama inavyooneshwa katika picha.

Hali hii ya kuwa jirani hutokea nadra sana.  Tukio la kusisimua kama hili halitatokea tena hadi July 2015 ambapo sayari hizi mbili zitakuwa jirani zaidi kwa mara tano ya zilivyo sasa hivi.

Jioni ya tarehe 25 na 26 Machi, Mwezi hilali mwembamba utaunganika na sayari hizi mbili na kutoa mandhari ya kuvutia mno katika anga za jioni.

Makutano ya Sumbula na Zuhura toka Pande Mbali Mbali za Dunia

Kati ya sayari nane (siyo tisa!) katika Mfumo wetu wa Jua, sita kati yao huonekana kwa macho bila kutumia darubini.  Kwa wakati huu sisi tunaweza kuona sayari tano kwa wakati mmoja.  Ukiangalia angani baada ya saa mbili usiku, Zuhura na Sambula zina tua katika upeo wa Magharibi.  Wakati huo, sayari ya Mirihi (Mars) inang’aa kwa rangi nyekundu kali upande wa Mashariki.  Wakati huo huo, sayari ya Zohali (Saturn) inaanza kuchomoza kwenye upeo wa Mashariki.

Advertisements

One thought on “Shuhudia Mpishano Adimu wa Sayari Zing’aazo Angani

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s