Je Kuna Maisha Nje ya Sayari ya Dunia?

Ukifuatilia vizuri utaona kuwa ulimwengu (universe) huu ni mkubwa mno; nadhani ni mkubwa kuliko uwezo wetu wa kufikiri na kuna maajabu mengi ambayo yamekuwa yakiwashangaza wanasayansi wote kiasi kuwa ni vigumu kujua ni nini kinaendelea. Ingawa hakuna anayeweza kusema kwa uhakika kabisa kutokana na uwezo wa kisayansi uliopo sasa; ila ni wazi kabisa kuwa maisha yameenea sana ulimwenguni na dunia hii ni sehemu ndogo tu ya uhai na maisha yaliyopo ulimwenguni.

Ulimwengu (The Universe)

Imeshathibitika sasa kuwa nyota nyingi zina; au karibia nyota zote zina mifumo ya sayari zinazozizunguka. Yaani kila nyota kama lilivyo jua ina mfumo wa sayari kama hizi zinazolizunguka jua. Vile vile utaalam unaonesha kuwa jua si nyota ya ajabu kuliko zingine, ni nyota ya kawaida tu; kwa maana kuwa ziko nyota nyingi tu, kwa mabilioni, zinazolingana na kufanana na jua. Ikiwa Uhai/Maisha unategemea nyota kama jua; basi nyota hizo zipo nyingi sana. Kwa nini basi nyota hizo nazo zisiwe na dunia zake kama ilivyo kwa jua?

Nyota (Stars)

Mazingira ya anga yanayozunguka eneo lilipo jua hayana tofauti na mazingira ya anga zinazozunguka nyota nyingine nyingi zaidi. Na hii si kwenye galaksia ya “milky way” tu bali hata kwenye galaksia nyingine kama “Andromeda”. Kumbuka kuna mabilioni ya galaksia zenye ukubwa na maumbo tofauti tofauti na kila galaksia moja ina nyota kwa mabilioni. Sasa hapa ni kitu gani kiifanye dunia kuwa kitu pekee? Hapa si suala la Mungu, kama Mungu yupo basi hakuumba dunia moja tu! Bali kaumba Matrilioni ya dunia yenye viumbe mbali mbali na tofauti tofauti. Uwingi wa uhai hapa duniani ni mfano tosha wa kutuonesha jinsi ulimwengu ulivyo tajiri wa uhai!

Uhai/Maisha duniani kwa kiwango kikubwa hutegemeana na uwepo wa jua. Kwenye mfumo wa jua huu tunaoufahamu (solar system) uhai umeshathibitika kuwepo hapa duniani; ambapo dunia ni mfano wa sayari yabisi (terrestrial or rocky plannets). Sayari nyingine ambazo zina ardhi kama dunia ni Zebaki (Mercury), Venus na Mars. Hata hivyo kuna satalaiti zinazozunguka sayari nazo ni yabisi au terrestrial. Mfano wa satalaiti hizo ni mwezi unaozunguka dunia; Lo, Ganymede, calypto na Uropa ambazo huzunguka sayari ya Jupiter; pamoja na satalaiti ya Titan inayozunguka sayari ya Saturn. Hata hivyo utaalam uliopo umeshathibitisha uhai kuwepo duniani tu.

Sayari nyingine kama Saturn, Jupiter, Uranus na Neptune zote ni sayari hewa (Gas giants). Yaani hazina yabisi kama ilivyo kwa hizo hizo sayari nne za kwanza yaani Zebaki, Venus, dunia na mars.

Sasa ikiwa kila jua lina mfumo wa sayari, ni wazi kati ya hizo zipo sayari yabisi kama zilivyo sayari za jua hili. Na kati ya sayari yabisi kuna uwezekano ikawepo moja au zaidi yanye uhai.

Sayari katika Mfumo wa Jua

Yaani kusema ukweli uhai hutegemeana sana na mfumo sahihi wa kikemikali (bio-chemistry). Mfumo wa kikemikali (Chemistry) hutegemeana sana na kuwepo kwa fizikia inayowezesha (enabling physics). Yamkini (Probability) ya kuwepo kwa fizikia inayowezesha kemia ya uhai kuwepo na hivyo uhai katika mifumo ya nyota nyingine ni kubwa mno.

Ukifanya tu mahesabu ya kidunia; katika nyota (yaani jua) moja kuna sayari nane. kati ya hizo, moja ina uhai. Yamkini ya uhai kwenye mfumo wa sayari yoyote hapa ndani ya mfumo jua (solar system) ni 1/8. Yaani ni asilimia 12.5. Kwa hiyo ukiwa na nyota nyingine kama jua yenye mfumo wowote wa sayari; kuna uwezekano wa kukuta uhai kwa asilimia 12.5. Sasa ukiangalia katika galaksia yetu ya milky way kuna nyota zaidi ya millioni 200 zilizo kwenye mazingira yanayofanana na yale lilipo jua; tena zenye ukubwa ulio sawa au unaokaribiana sana na jua. Nyota zote zilizo karibu na jua zimeshathibitika kuwa na mfumo wa sayari tayari!

Milkway Galaxy

Kwa hiyo ikiwa kuna asilimia 12.5 ya kukuta uhai katika kila nyota inayofanana na jua; katika nyota millioni 200 zinazofanana na jua, ndani ya galaksia ya milky way kuna nyota milioni 25 zenye uhai!!!!!!!

Yaani Nyota milioni 25 zina uhai ndani ya Galaksia moja tu ya milky way!! Changamoto ni kuutafuta. Tena ni uhai ule ule kama huu uliopo duniani.

Last edited by KipimaPembe; 7th February 2012 at 09:04  (Imechukuliwa kutoka Jamii Forum na picha zimeongezwa na Mponda Malozo)

Advertisements

17 thoughts on “Je Kuna Maisha Nje ya Sayari ya Dunia?

 1. sir fuya mwanga says:

  ni kwambaaa katika sayri ,kuna aina moja ya sayari inayosadikika kua huweza ikawa viumbe hai wakaishi
  katika hiyo sayari kuna maji mengi ya kutosha na kubakiwa na asilimia chache ya nchi kavu
  embu chunguza vizuri

  • unawetanzania says:

   Sayari zipo nyingi na zinazidi kuzinduliwa kila siku ingawa zote hizo zipo nje ya mfumo wetu wa Jua. Sayari hizo zina sifa mbali mbali lakini hadi leo hii wanasayansi hawajaweza kuona maisha katika sayari hizo kama tunavyoyajua sisi. Ingawa dalili muhimu zinazoweza kupelekea maisha zinaweza kuwepo kama vile uwepo wa maji na kaboni.

  • unawetanzania says:

   Habari Halifa, jibu ni hapana kwani hata zikiwa katika mstari mmoja na Jua, hizo sayari bado zipo mbali sana kati yao. Hivyo haziwezi kuwa na uwezo wa kuzuia mwanga wa Jua na kusababisha kuwepo kwa giza la muda mrefu.

 2. Mwl.teacher says:

  Ni vitu gani zaidi vinapelekea maisha yapatikane sayari moja tu ambayo ni dunia na siyo katika sayari zingne????

  • unawetanzania says:

   Hatuwezi kusema kwa uhakika kuwa hakuna maisha katika sayari nyingine, kwani kuna sayari nyingi sana katika ulimwengu na hasa nje ya mfumo wa Jua. Hadi sasa binadamu ameweza kutuma vyombo vya kuchunguza sayari zilizomo katika mfumo wa Jua peke yake na katika hizo kuna dalili za kuwepo viashiria vya maisha kama uwepo wa maji katika sayari ya Mars. Si rahisi kwa sayari kuwa na viashiria vyote vya maisha kama vilivyopo katika sayari ya Dunia, hali inayopelekea wanasayansi kudhani kuwa hata kama kuna maisha katika sayari hizo, basi yatakuwa tofauti na maisha tuyajuayo sisi katika sayari yetu ya Dunia. Vitu vinavyopelekea uwepo wa maisha katika sayari yetu kama tuyajuavyo ni hewa ya Oxygen, Carbon dioxide au hewa ya ukaa pamoja na jamii.

  • unawetanzania says:

   Ukweli ni kuwa hakuna uhakika uliwahi kutolewa kuhusu uwepo wa viumbe hao Duniani, ila kuna simulizi za watu mbali mbali zinazoelezea kuwepo kwa watu hao ingawa simulizi hizi hazijathibitishwa na vyombo vya uhakika. Hivyo, tunaweza kusema kuwa viumbe hao hawapo.

 3. twaha bashiri says:

  binafsi nimekuwa nikisoma sana machapisho mbalimbali ya kisayansi kutaka kujua kama kuna viumbe vingine na uhai katika sayari nyingine lakini mpaka sasa hakuna tafiti hata moja imethibitisha kuwa kuna viumbe vinapatikana katika sayari nyingine

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s