Mizunguko ya Sayari na Mabadiliko yake Angani

Anga kama moja ya zana kuu za udadisi zitaendelea kutupatia mandhari ya kukuza udadisi wetu wakati wa jioni mara baada ya kuchwa kwa Jua katika ya miezi kadhaa ijayo hadi mwezi Mei mwakani. Sayari mbili zitakazoonekana kamanyota kali upande wa  Mashariki na Magharibi ni sayari ya Zuhura (Venus) na Sumbula (Jupiter).

Kwa wakati huu Zuhura inaonekana upande wa magharibi mara tu baada ya kuzama kwa Jua, na sayari ya Sumbula nayo inachomoza upande wa Mashariki na sayari zote mbili zitakuwa zinakwenda juu angani kadri siku zinavyokwenda, na sayari hizi zitabadilisha nafasi zao kadri siku zinavyokwenda na kufanya Sayari ya Sumbula kuonekana juu kabisa utosini huku sayari ya Zuhura ikibadilisha mahali lakini bila kufikia utosini.

Mabadiliko mbali mbali ya sura ya sayari ya Zuhura yanayofanana na mabadiliko ya umbo la Mwezi yatatokea wakati Zuhura ikijizungusha katika mzingo wake (orbit). Mabadiliko haya huonekana kwa kuangalia sayari hii kwa kutumia darubini ndani ya miezi saba ijayokama inavyoonekana kwenye mchoro.

Kutokana mzunguko wa Zuhura wakazi wa Dunia wataweza kuona tukio la kipekee la Zuhura kukatana na Jua tarehe 6 Juni 2012 hali ijulikanayo kisayansi kama “Mpito wa Zuhura Juani” (Transit of venus). Tukio ambalo halitajirudia maishani mwetu kwani litajirudia tena mwaka 2117. Wakazi waTanzaniawaweza kuona hali hii asubuhi ya tarehe 6 Juni wakati Jua likipambazuka.

Mwendo halisi wa Sayari mbiguni unaweza kushuhudiwa kwa kuangalia mkutano wa karibu wa sayari, nyota na Mwezi, ambapo tangu mwanzo wa mwezi ulipita sayari ya Zebaki (Mercury) iliisogelea sayari ya Zuhura na  10 Novemba zilikukutana kwenye kundi la nyota la Nge (Scorpion) na kuungana na nyota kubwa nyekundu ya Antares na kutengeneza mwonekana wa kuvutia kama invyoonekana kwenye picha.

Wakati sayari zikiendelea kutembea angani, tarehe 26 Novemba anga itakuwa na mwonekano wa kuvutia ambapo sayari ya Zebaki na Zuhura zitakuwa pembezoni mwa Mwezi mwandamo na siku inayofuata sayari hizi zitakuwa zimeshuka chini ya Mwezi mwandamokamainavyoonekana katika picha hizi.

Na kwa kuwa Sayari ya Zebaki ipo kwenye mzingo wa ndani wa mzingo wa Dunia kama iliyo Zuhura nayo itaanza kuwa na mabadiliko ya sura ukiiangalia kwenye darubini na hii itakuwa ni fursa nzuri ya kutumia darubini kuangalia mabadiliko ya haraka katika sura za hilali, hali ambayo ni adimu.

Tafadhali bonyeza linki hapo chini kupata taarifa za kina kuhusu taarifa hii na majibu ya maswali yako kwa kutumia hesabu na sayansi.

** The Kiswahili version is available at https://sites.google.com/site/astronomyintanzania/previousmonthsnightskies/mabadiliko-katika-mwonekano-wa-zuhura-angani

**you can also point to the English version which is at this website:  https://sites.google.com/site/astronomyintanzania/previousmonthsnightskies/varying-views-of-venus

Advertisements

3 thoughts on “Mizunguko ya Sayari na Mabadiliko yake Angani

    • unawetanzania says:

      Ni kweli kuwa Jua ni nyota na kutokana na kuwepo kwa nyota nyingi ulimwenguni wanasayansi waanaamini kuwepo kwa uhai katika nyota nyingine ingawa bado hawajaweza kuthibitisha hadi leo kutokana na nyota hizo kuwa mbali mno, hivyo kushindikana kwa uwezo wa kuzifikia. Lakini wameweza kugundua sayari nyingi ambazo zipo nje ya mfumo wetu wa jua na ambazo zinazunguka nyota nyingine. Tunashukuru sana kwa swali lako na kama una swali jingine karibu kuuliza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s