Sikukuu ya Eid el Fitr na Udadisi-Mwezi

Watu wenye kufuata imani ya dini ya kiislamu katika jamii, wamekuwa wakipata mkanganganyiko wa mawazo juu ya siku halisi za siku kuu zao. Kutokana na kukosa uhakika wa siku halisi watu wengi wamekuwa wakishindwa kupanga mipango katika siku ambazo sikukuu zinatarajiwa.

Kupitia vilabu vya sayansi vilivyoanzishwa na UNAWE-Tanzania , elimu ya sayansi ya anga na udadisi wa watoto, tunaweza kuangalia kwa pamoja ni vipi tunaweza kufahamu siku halisi za sikukuu za kiisalamu kwa kuanzia na sikukuu ya Eid el Fitr mwaka 2011.

Watoto wakidadisi Anga Mwanza

Kalenda ni kipimo cha mda kinachotumika na mwanadamu kuweza kupanga ratiba mbali mbali za mwaka. Pia kalenda zipo za aina nyingi na hutofautiana kulinga na tamaduni tofauti tofauti duniani, ili kuondoa mkanganyiko baina ya watu wa tamaduni tofauti kalenda ya Gregorian (Kalenda ya Sasa) ilianza kutumika zaidi bara la Ulaya baadae kusambaa sehemu kubwa ya Dunia likiwemo bara la Afrika.

Wakati sehemu zingine wanatumi kalenda ya Gregory waarabu waliendelea kutumia kalenda yao iliyokuwa ikifuata mzunguko wa mwezi na hivyo kufanya waumini wa kiislamu kuendelea kuifuta kalenda hiyo kwa shughuli mbali mbali za imani yao.

Kalenda inayofuata Mzunguko wa Mwezi

Mwezi huzunguka sayari ya Dunia kwa siku 29 au 30 na hivyo kufanya miezi ya kalenda ya kiislamu kuwa na siku 29 au 30 na si 28 kwa mwezi wa pili au 31 kama ilivyo katika kalenda ya Gregory. Ili kuweza kutambua tarehe na siku sahihi katika imani ya kiislamu basi waislamu hawana budi kufutilia mzunguko wa mwezi kila siku.

Wanasayansi na wana anga wamekuwa wakifuatilia mzunguko wa mwezi na hata kuweza kutengeneza program za komputa zenye uwezo wa kutambua mzunguko wa mwezi na hivyo kufahamu tarehe halisi za sikukuu mbali mbali zilizopo kwenye imani hiyo.

Waislamu wengi wamejawa na shauku ya kujua ni lini itakuwa sikuu ya Eid. Je ni tarehe 30 au 31? Kufahamu hilo tuanza kuangalia mzunguko wa mwezi kwa pamoja

Tarehe 29/08/2011 alfajiri (Saa 12:04 asubuhi) mwezi utakuwa katikati ya Jua na Dunia, mpangilio ambao unaashilia kuanza kwa mwezi mpya (mzunguko mpya). Kufikia jioni siku hiyo mwezi utakuwa umesogea umbali wa nyuzi 6 katika kizio cha magharibi cha Dunia. Jioni hiyo itawawia vigumu watu kuweza kuona mwezi huu mchanga sana katikati ya mwanga wa jua la machweo upande wa magharibi wa Dunia yetu, na mara baada ya Jua kuzama kutakuwa na dakika 20 tu kabla ya mwezi huu mchanga nao kuzama na kupotea kwenye macho ya watazamaji.

Mwezi Mwandamo na Mwanga wa Jua la Machweo

Machweo tarehe 30/08/2011 yatatokea wakati mwezi ukiwa umeshasogea umbali wa nyuzi 12 na kupanda juu kwa nyuzi 17. Hali hii itatoa mda mwingi kati ya Jua kuzama na kufanya anga liwe na giza, pia kuufanya mwezi uwe juu nyuzi 10 kutoka katika kizio cha magharibi. Kutokana na hali hiyo watu wataweza kuuona mwezi mchanga kwa mda mwingi kabla haujazama saa moja na nusu jioni. Mwezi pia unatarajiwa kuwa karibu kabisa na Dunia siku hiyo na hivyo kuufanya uonekane mkubwa na kwa urahisi.

Kutokana na imani ya kiislamu inayoeleza kuwa waumini wake watafunga na kufungua kutokana na kuonekana kwa mwezi mwandamo, hii itawapelekea waislamu wengi wanaofuata maagizo hayo kutekekeleza sikukuu hiyo siku ya tarehe 31/08/2011.

UNAWE-Tanzania inawatakia Eid Njema Watoto Wote

Advertisements

4 thoughts on “Sikukuu ya Eid el Fitr na Udadisi-Mwezi

 1. Amani Athumani Herry says:

  Asante ndugu yangu Mponda kwa elimu nzuri ya kuandama kwa mwezi na ufafanuzi juu ya sikukuu za kiislamu,
  Kuna watu ambao wanaishi Tanzania lakini wanafungua na kufunga kwa kufuata mwezi unaoandama katika za Kiaarabu, Je watu hawa wako sahihi, au unaweza kuishi Tanzania kutokana elimu ya Astronomia ikawezekana kufuata kalenda ya mwezi ya bara lingine?

  • unawetanzania says:

   Habari Mr. Amani na napenda kushukuru kwa maswali mazuri. Kwa ufupi ni vizuri watu wakatumia elimu ya sayansi waliojaliwa kuwa nayo, kuongezea na elimu yao ya anga ili kuweza kutafakari ni jambo lipi sahihi kwao kulingana na udadisi wao au wa mtu binafsi.

 2. Mbusule Christopher says:

  Asante sana kwa elimu hiyo nzuri,kulikuwa na mkanganyiko mkubwa sana&pengine wengi 2liamini ingekuwa tar.30/08/11. Ckuku njema!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s