Tumeona Mwezi Ukisogea

Kutokana na tukio la kupatwa kwa Mwezi la tarehe 15/06/2011 kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuwa tumejifunza. Moja kati ya mambo hayo ni utabiri halisi wa tukio zima. Watu wengi wanaweza kuwa wamestaajabishwa na jinsi mda ulivyoweza kutabiriwa hata kabla ya tukio lenyenyewe.

Tukio zima liliweza kutabiriwa kutokana na kufahamu mzunguko wa Mwezi upokuwa unaizunguka Dunia katika mhimili wake (Orbit), tunaweza pia kuuliza ni uhusiano gani uliopo kati ya mda halisi wa tukio la kupatwa kwa Mwezi na ufahamu wa mzunguko wake. Uhusiano na ufahamu wa tukio zima unaweza kuelezewa kwa kufahamu mzunguko wa mwezi.

Kukokotoa Mzunguko wa Mwezi

Mwezi huchukua mda wa mwezi mmoja takribani siku 30 kuzunguka Sayari ya Dunia katika mhimili wake ambao unatengeneza nyuzi 360ndani ya siku hizo 30. Hii ina maaanisha kwamba Mwezi hutembea nyuzi 12o kwa mda wa siku moja, iliyopatikana kwa kugawanya nyuzi 360o kwa siku 30 za Mwezi mzima.

Ili kutambua ni nyuzi ngapi mwezi unatembea ndani ya lisaa limoja itabidi ugawanye nyuzi 12o kwa masaa 24 ambayo yanatengeneza siku moja. Hapa utapata  nusu nyuzi (0.5o) ambazo Mwezi huzunguka Dunia kwa mda wa lisaa limoja kama ilivyoweza kuonekana wakati ya kupatwa kwa Mwezi.

Hii inamaanisha kwamba tulikuwa tunaangalia mwezi ulivyokuwa unasogea taratibu angani na kukatiza katika kivuli cha Dunia. Wakati wa tukio hili kizio cha mashariki cha mwezi kilikuwa cha kwanza kufunikwa na kivuli cha sayari ya Dunia na hii inadhihirisha kwamba Mwezi unaizunguka Dunia kutoka Magharibi kuelekea Mashariki.

Unaweza kuthibitisha hili kwa kuangalia jinsi mwezi mchanga (New moon) unavyochomoza upande wa Magharibi wakati jua linapochwea. Na jinsi siku zinavyokwenda Mwezi huo huchomoza juu na juu zaidi ya siku iliyopita na baada ya siku 7 mwezi unakuwa juu yetu na kutengeneza umbo la nusu Mwezi.

Baada ya siku 14 wakati wa Jua kuchwea Mwezi huo huchomoza upande wa Mashariki kama Mwezi mpevu (full moon). Hii  inamaanisha kwamba ndani ya siku 14 kutokea Mwezi mchanga hadi mwezi mpevu mwezi unakuwa umesogea kutoka Mashariki kuelekea Magharibi

Vitu vyote vilivyomo angani pamoja na sayari zote vinasogea taratibu kila siku kuelekea upande wa magharibi na hii ni tabia ya asili ya mfumo wetu wa Jua. Hivyo basi wakati tulipokuwa tunaangalia kupatwa kwa Mwezi tulikuwa tunaangalia jinsi mwezi ulivyokuwa unasogea kutoka Mashariki kuelekea upande wa Magharibi na kukatiza katika kuvuli cha sayari yetu ya Dunia.

Je haikupendeza kuangalia jinsi Mwezi ulivyokuwa unasogea? Angalia tena katika video hii hapa

Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye barua pepe ya Dr. Jiwaji akijibu swali la wanafunzi wa Agape Secondary iliyopo Moshi Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s