Kupatwa Kwa Mwezi Funzo La Sayansi

Usiku wa Jumatano tarehe 15/06/2011 kuanzia saa 3: 23 usiku hadi saa 7:03 usiku Watanzania wataweza kushuhudia tukio la mwezi kupatwa ambapo Sayari yetu ya Dunia itakuwa katika mstari mmoja pamoja na Jua na Mwezi.

Tukio hili ni adimu katika karne hii kwani Mwezi utafunikwa kabisa na kivuli cha sayari yetu ya Dunia na mara ya mwisho tukio hili lilitokea miaka arobaini iliyopita tarehe 6/08/1971. Kipindi hicho wengu wetu tulikuwa hatujazaliwa na hata waliokuwepo ni wachache walioweza kutambua ni nini kilichokuwa kinaendelea.

Picha ya Kupatwa kwa Mwezi

Kupatwa huku kutatokea wakati mwezi ukiwa mpevu (full moon) ambapo mwezi utachomoza saa 12:03 jioni kabla ya jua kuzama na masaa matatu baadae saa 3:22 usiku upande wa mashariki wa mwezi utaanza kupokea taratibu kuvuli cha sayari ya Dunia.

Baada ya lisaa limoja saa 4:22 usiku mwezi mzima utakuwa umemezwa katika kivuli cha Sayari ya Dunia na hapa ndio utakuwa mwanzo wa kupatwa kamili kwa mwezi (Total Lunar Eclipse). Mwezi utapita katikati ya kipenyo cha kivuli cha sayari ya Dunia na ifikapo saa 5:02 usiku utakuwa katikati ya kivuli kinene cha sayari Dunia na kusababisha kiza kinene kinachoashiria kupatwa kamili kwa mwezi kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita.

Mwezi utakuwa umezingirwa katika kivuli cha sayari ya Dunia hadi saa 6:03 na baada ya hapo sehemu ya upande wa mashariki ya mwezi itaanza kutoka katika kivuli cha Dunia na tukio hili litaendelea kwa lisaa limoja hadi saa 7:02 usiku ambapo mwezi utakuwa umeondoka katika kivuli cha Dunia na kurudia katika hali yake ya kawaida.

Picha ya kuonyesha mda wa kupatwa kwa Mwezi

Tukio hili la pekee ni funzo la sayansi kwa watoto, wazazi na jamii yote kwa ujumla kwani wengi wetu hatufahamu wala kuamini kama ni kweli Dunia inaelea na kuzunguka Jua na pia ni vigumu kwetu sisi kufahamu jinsi mwezi unavyoizunguka sayari ya Dunia.

Kutokana na tukio hili tunaweza kujiuliza maswali mengi na kuhisi ni jinsi gani tulivyo na uhusiano wa karibu na anga yetu. Kupatwa kwa Mwezi hutokea pindi sayari ya Dunia, Nyota ya Jua na Mwezi vinapokuwa katika mstari mmoja vikiwa katika mizunguko yake.

Sayari ya Dunia inazungukwa na Mwezi kwa siku takribani 27 au 29 na kufanya mwezi mmoja wa kalenda na Mwezi pamoja na Dunia vinazunguka Jua kwa siku takribani 365 na kufanya mwaka mmoja wa kalenda. Dunia na Mwezi vinazunguka jua katika nyuzi (angle) mbali mbali na kusababisha matukio ya kupatwa kwa Mwezi na Jua kutokea mara chache.

Jua ni chanzo pekee cha mwanga katika mfumo wa Jua hivyo na hivyo hutengeneza kuvuli kwenye uso wa Mwezi pale sayari yetu inavyokatiza katikati yake na mwezi katika mstari ulio nyooka na kufanya tuone kivuli cha sayari yetu kwenye uso wa mwezi. Hii inadhihirisha kwamba sisi na Sayari yetu tupo kwenye mwendo siku zote za maisha yetu na nguvu ya uvutani (Universal Gravitational Force) ndio inatushikilia hapa tulipo.

NB: Baadhi ya maneno yametafsiriwa kutoka kwenye Makala ya Dr. Jiwaji iitwayo Darkest Total Luna Eclipse 14/06/2011 na pia picha ya mda wa kupatwa kwa Mwezi imetolewa huko.

Advertisements

6 thoughts on “Kupatwa Kwa Mwezi Funzo La Sayansi

 1. hans kiwoli says:

  ni bora imetokea usiku manake ingetokea mchana bongo pasingekalika watu wangedhani ndio mwisho wa dunia kama walivyotudanganya last month

 2. farida mnzava says:

  natamani ingetokea mchana ili ionekane vizuri japokua wale ambao hawana elimu juu ya tukio hili wangekua na hofu kubwa

 3. Zidiel says:

  Je,dunia uzunguka ndan au juu.na kama n juu mbona binadamu atuzunguki kwan na sisi situpo juu ya dunia nini usababisha ivyo.?

  • unawetanzania says:

   Habari Zidiel na tunashukuru kwa swali lako zuri. Jibu lake ni kwamba Dunia hujizungusha katika muhimili wake na wakati huo huo hulizunguka jua, hivyo basi Dunia huzunguka juu. Je kwanini sisi hatuzunguki? Ili kuweza kujua kama unazunguka huna budi kuwa na kielelezo kingine cha kukuonyesha kama unazunguka au kutembea. Mfano kama ukiwa kwenye gari utajua kama unatembea pale utakapokuwa unavipita vitu na kuviacha nyuma. Sasa ukija katika Dunia kielelezo chetu ni jua na nyota ambavyo hubadilika kila usiku na pia kati ya mchana na jioni kutokana na kuzunguka huku kwa Dunia. Hivyo anza kuvichunguza ili kujua kuwa tunazunguka. Je ni nini husababisha hivyo? Jibu lake hapa ni nguvu ya uvutano ndio inayosababisha dunia kuzunguka pamoja na vitu vyote vilivyopo huko angani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s