Kukatiza Kwa Zuhura (Venus) na Mwamko wa Sayansi Tanzania

Tarehe 6/6/2012 kutatokea tukio la sayari ya Zuhura (Venus) kukatiza katikati ya Jua na sayari yetu ya Dunia. Tukio hili ni tukio adimu sana katika maisha ya mwanadamu kwani hutokea mara moja ndani ya karne moja (miaka mia moja).

Mchoro wa kuonyesha Jua, Zuhura na Dunia katika mstari mmoja

Sayari ya Zuhura ilikatiza katikati ya Jua na Dunia mara sita tangu darubini ilipozinduliwa miaka 400 iliyopita na wanasayansi katika karne ya 18 na 19 walisafiri sehemu mbali mbali Duniani ili kuona jinsi sayari ya Zuhura inavyokatiza Jua na kukokotoa umbali wa sayari ya Dunia kutoka kwenye Jua na mwishowe kupata ukubwa halisi wa mfumo wa Jua. Katika karne ya 18 na 19 wanasayansi walichukua karibu karne nzima ili kuweza kufanikinsha lengo la kuangalia tukio hili kutokana na kuwa na teknolojia duni za kusafiri na mawasiliano.

Mchoro wa kukatiza kwa Venus mwaka 1882

Leo hii Dunia ina historia ya mchanganyiko wa tamaduni mbali mbali kutokea katika enzi za Wagiriki zinazoelezea kalenda, umbali wa Dunia kutoka kwenye Jua na ukubwa wa mfumo wa jua. Katika karne hii ya 21 Astronomy Without Borders wameandaa programu maalum kwa ajili ya wanafunzi na jamii yote kwa ujumla kuweza kushiriki katika kukokotoa umbali wa Dunia na ukubwa wa mfumo wa jua wakati wa kukatiza kwa sayari ya Zuhura. Programu hii maalum itazinduliwa katikati ya mwaka 2011 na wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla wanaweza kushiriki kwa kutumia simu za mkononi, mtandao wa intaneti na njia nyingine za asili.

Picha ya Zuhura ikiwa kati kati ya Dunia na Jua

Tukio hili lina umuhimu wa kipekee kwa jamii ya watanzania kwani kwa mda mrefu tumekuwa na maswali mengi juu ya sayansi ya anga na kutofanikiwa kufahamu umuhimu wake katika jamii yetu. Kutokana na tukio hili tutaweza kutambua ni jinsi gani tunaweza kutumia hesabu, uvumbuzi wa darubini (telescopes), kutambua chanzo cha hesabu, kwa sababu gani zilivumbuliwa na tunawezaje kuzitumia katika mazingira yetu ya kila siku.

Ramani ya Dunia Kuonyesha Sehemu ambazo Zuhura itaonekaTutakuwa na uwanja wa kuuliza maswali mengi kuhusu anga na kufahamu ni jinsi gani mababu zetu walikuwa wakiitumia na ni kwa njia zipi tunaweza kuchanganya ufahamu wao na sayansi ya sasa ili kuongeza mwamko wa sayansi katika jamii yetu na pia kutambua mchango na thamani ya sayansi ya asili ya Afrika.

Kwa taarifa zaidi juu ya tukio hili tafadhari tembelea tovuti  http://www.transitofvenus.org/ na kwa maswalii zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia njia hizi https://unawetanzania.wordpress.com/contact-us-2/

Advertisements

2 thoughts on “Kukatiza Kwa Zuhura (Venus) na Mwamko wa Sayansi Tanzania

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s