Kupatwa Kwa Jua Wakati wa Mstarini

Tarehe 15 Januari 2010 anga itaonyesha tukio la kupendeza kuanzia saa moja na dakika saba hadi saa tano na dakika kuminasaba asubuhi.Tukio hili litatokea wakati shule nyingi zitakuwa zimejikusanya mstarini asubuhi, ambapo itaongeza idadi ya watu watakoshudia hususani ni watoto. Sehemu kubwa ya Jua itakingwa na Mwezi wakati wa kupatwa kwa Jua. Tanzania hatutaweza kuona duara (pete) la Jua siku hiyo, lakini tutaweza kuona Jua likiwa limefichwa kiasi kikubwa, kama asilimia 80 hadi 90. Hali hii itasababisha mabadiliko makubwa ya mwanga wa asubuhi siku hiyo, utadhani wingu nene limefunika Jua, hata kama anga hakutakuwa na mawingu.Watu wa Uganda na Kenya na walio ukanda wa bahari ya Hindi kuelekea India na China wataweza kuona Jua likiwa limefunikwa na Mwezi ila mduara mwembamba wa mwanga utabaki unang’aa kama pete.

 Wakati wa kupatwa Jua, Mwezi huwa unakaa katika mstari mmoja kati ya Dunia na Jua. Kutoka Duniani tunaona kupatwa kwa Jua kwa vile Mwezi umekinga mwanga wa Jua. Wakati wa kupatwa kwa jua usijaribu kuangalia jua kwa macho bila miwani maalum ya kulinda macho (USIJARIBU KUANGALIA JUA MOJA KWA MOJA NA MACHO YAKO = USIFANYE HIVYO KABISA LA SIVYO UTAPOTEZA MACHO!). Tunapenda kuwashauri watu watumie miwani ya kuchomelea (welding) kwani hiyo ndio mizuri ambayo haina athari. Njia mbadala ni kutumia vioo vilivyofunikwa vizuri na weusi wa masizi (carbon soots) ya mshumaa au koroboi. Carbon soot iwe katikati ya vioo viwili vilivyobanwa vizuri kwa gundi. Ni muhimu kujaribisha vioo hivi kabla ya kuruhusu kuvitumia

 UNAWE Tanzania ikishirikiana na EWAT itafanya mafunzo ya kuvumbua anga (Kids Sky Exploration) Jumamosi ya Tarehe 16, ambayo ni siku moja baada ya tukio la kupatwa kwa jua katika Shule ya Msingi Solomoni Mahlangu iliyopo Mazimbu Morogoro. Tukio hili litawaleta pamoja watoto wa Kampasi ya Solomoni Mahlangu na wale wa jirani, dhumini kubwa likiwa ni kuongeza uelewa wao juu ya matukio ya kupatwa kwa Mwezi na |Jua yaliyotokea mwishoni na mwanzoni mwa Mwaka

 UNAWE Tanzania na EWAT inawakaribisha washikadau wote na watu wenye mapenzi mema kushiriki katika tukio hili pia kuwapa zawadi watoto kama njia ya kuongeza shauku yao katika sayansi.

 Na Mponda Malozo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s