Anga kuzawadia watoto usiku wa mwaka mpya

Ingawa mwaka huu ulikuwa si wa matumaini kwa wale wanaopenda kuona kupatwa kwa Jua na Mwezi, lakini hawatovunjwa moyo moja kwa moja. Usiku wa mwaka mpya anga itawazawadia zawadi ya kupatwa kwa Mwezi na zawadi kubwa zaidi itatolewa na anga wiki mbili baadae.

Tarehe 31 Desemba kutakuwa na Mwezi mpevu utachoza upande wa mashariki mara tu baada ya Jua kutua upande wa magharibi.  Usiku huo, sehemu ndogo ya Mwezi, kiasi kama asilimia nane (8) hivi kitafichwa gizani kutokana na kupatwa kwa Mwezi. Kabla tu ya saa nne usiku yaani saa 3:53 usiku, wakati Mwezi ukiwa Mashariki nusu ya safari yake angani, Mwezi utaanza kufunikwa kutokea chini na kivuli cha sayari ya Dunia. Baada ya nusu saa, yaani saa 4:30 usiku kiasi cha asilimia nane (8) hivi ya Mwezi itakuwa imefunikwa na kivuli cha Dunia. Baada ya nusu saa nyingine, yaani saa 4:53, kivuli cha Dunia kitkuwa kimeaondoka kwenye uso wa Mwezi kutokea sehemu ya juu ya Mwezi na Mwezi utabaki ukiwa mpevu tena. Hakika hii ni zawadi kubwa kabisa usiku wa kukaribisha Mwaka Mpya 2010.

Tukio jingine kubwa zaidi tunalisubiri wiki mbili baadae, yaani tarehe 15 Januari 2010 saa moja na dakika saba hadi saa tano na dakika kuminasaba asubuhi. Sehemu kubwa ya Jua (takriban zaidi ya silimia 80%) itakingwa na Mwezi wakati wa kupatwa kwa Jua. Watu wa Uganda na Kenya na walio ukanda wa bahari ya Hindi kuelekea India na China wataweza kuona Jua likiwa limefunikwa na Mwezi ila mduara mwembamba wa mwanga utabaki unang’aa kama pete. Hapa Tanzania hatutaweza kuona duara (pete) la Jua siku hiyo, lakini tutaweza kuona Jua likiwa limefichwa kiasi kikubwa, kama asilimia 80 hadi 90. Hali hii itasababisha mabadiliko makubwa mwanga wa asubuhi siku hiyo, utadhani wingu nene limefunika Jua, hata kama anga halitakuwa na mawingu.

Wakati wa kupatwa kwa Mwezi, Dunia huwa inakua katikati ya Mwezi na Jua, lakini wakati wa kupatwa kwa Jua, Mwezi huwa unakaa katika mstari mmoja kati ya Dunia na Jua. Kutoka Duniani tunaona kupatwa kwa Jua kwa vile Mwezi umekinga mwanga wa Jua. Lakini inawezekanaje wakati tunaelewa kuwa Mwezi ni mdogo mara 400 ukilinganishwa na Jua? Jibu linapatikana ukizingatia kwamba Mwezi pia upo karibu na Dunia mara 400 ukilinganisha na Jua. Hali hii inatufanya tuone Mwezi na Jua vinafanana kwa ukubwa angani. Kawaida hatuwezi kutambua uwiano huu kwa kuangalia Jua moja kwa moja kwani mwanga wa Jua unaweza kukupofua ukiangalia Jua moja kwa moja (USIJARIBU KUANGALIA JUA MOJA KWA MOJA NA MACHO YAKO = USIFANYE HIVYO KABISA LA SIVYO UTAPOTEZA MACHO!) lakini ukiwa na mawani maalum unaweza kuona kwa urahisi zaidi uhusiano huu kati ya ukubwa wa Mwezi na Jua.

UNAWE Tanzania, inayohusiana na kuhamasisha mwamko wa uelewa Ulimwengu wetu, itakuwa na furaha kusherehekea zawadi hizi mbili za mwaka mpya itakayotolewa na anga yetu pamoja na watoto wote wa Tanzania. Watoto wanaokaa karibu na Stakishari Ukonga, Banana wataweza kujumuika na Mponda Malozo, wanaokaa karibu na Mbezi Sacuveda wanaweza kujumuika na Joeline Ezekiel, wanaokaa karibu na Solomoni Mahlangu Morogoro wanaweza kujumuika na Deodatus Kiriba. Shule ya Msingi Milama Mvomero watasaidiwa na mwalimu wao mkuu jinsi ya kushiriki na shule zilizopo Monduli Mjini, na zilizotembelewa na UNAWE Tanzania watasaidiwa na Essau Loisujaki jinsi ya kutekeleza matukio haya.

UNAWE Tanzania inapenda kuwasihi walimu wote wa Sayansi, wafalaki chipukizi na watu wenye shauku ya kutazama anga kushiriki katika tukio hili na kufanya watoto wengi zaidi wa Tanzania waweze kuangalia maajabu ya anga na pia kuibua shauku yao kwenye masomo ya sayansi na anga.

Pia tembelea http://sites.google.com/site/astronomyintanzania/

Na Mponda Malozo na Noorali Jiwaji

DOKEZO:

Wakati wa Kupatwa kwa Jua na Mwezi ni mda mzuri wa kuibua shauku za watu kutazama anga, lakini wanatakiwa waandaliwe na kufahamu kuwa sehemu ndogo tu ya mwezi ndio itakuwa imepatwa.

Hata hivyo sehemu nyeusi ya Mwezi iliyopatwa itaonekana katikati ya tukio hili mnamo saa 4: 30 usiku. Hivyo kwa umakini zaidi fuatilia mmuliko wa mwezi kabla na baada ya kupatwa kwa Mwezi. Na hii itakuwa vizuri zaidi kama anga itakuwa na mawingu mengi.

Tovuti zifuatazo ni nzuri kuwaandaa watu kuangalia kupatwa kwa mwezi na nini cha kutarajia.

http://en.wikipedia.org/wiki/File:Lunar_eclipse_chart_close-2009Dec31.png

http://www.timeanddate.com/eclipse/lunar-eclipse-december-31-2009.html

http://www.jodrellbank.manchester.ac.uk/astronomy/nightsky/Eclipse2.jpg

Tovuti hii ifuatayo itakuonyesha jinsi mwezi unavyotembea, pia kupatwa kwake. Pia utapata taarifa za kupatwa kwa Jua tarehe 15 January.

http://www.shadowandsubstance.com/

Advertisements

2 thoughts on “Anga kuzawadia watoto usiku wa mwaka mpya

  1. Albert M Kisongola says:

    Am happy to get the information on the eclipses.It is another chance for the world to shopw its wonders and the science it carries.
    On the night of New Year i’ll be with my family and neighbours looking at the sky and on 15th Jan am hoping to help Mr Mponda running the issue.
    MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR TO ALL

    By Albert M Kisongola.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s