Timu A ni ya Kimataifa

Katika kila pande ya Dunia kuna wanaanga wanashughulika. Baadhi yao wanafanya kazi katika vituo vya kuchungaza anga vya kiastronomia, wengine wanafanya kazi katika vyuo vikuu au katika taasisi za utafiti.

Picha hii inaonyesha kituo kipya cha kuchunguza anga kilichopo Uholanzi, kiitwacho LOFAR. Awali Kilikuwa kinafanya kazi ya kuchunguza vitu ambavyo bado havijavumbuliwa katika ulimwengu. Mamia ya wanasayansi wanaanga kutoka katika pande mbali mbali za Dunia wamekuwa wakikitumia kituo cha LOFAR kwa shughuli zao za utafiti.

Wanaanga hawa hufanya kazi kwa pamoja kutoka sehemu mbali mbali Duniani na hutumia zana za mtandao (online tools), kama barua pepe na simu za video. Pia hupanga kutembeleana katika ofisi zao na kukutana katika mikutano ya kimataifa ya astronomia. Pindi wanapofanya ugunduzi, wanaanga huchapisha uvumbuzi wao kama timu moja.

Kwa mfano, chapisho la karibuni kutoka LOFAR lilihusisha timu kubwa ya wanaanga 84 kutoka katika vyuo na vituo vya utafiti 26 vilivyopo katika nchi 9! Walitumia LOFAR kuchunguza kundi la galaxi lililoitwa galaxy cluster (mkusanyiko wa galaxi). Timu hii iliona kuwa mawimbi redio yanayotoka katika galaxi cluster yalikuwa makali kuliko walivyotarajia. Walifikiri ni kwa sababu yalikuwa yakikinzana na mkusanyiko mdogo wa galaxi.

Wanaanga hawa wamesambaza ugunduzi huo mpya na kwa wanaanga wengine wote Duniani. Wanaanga  hufanya kazi kwa pamoja na hubadilisha mawazo wakutanapo katika mikutano ya kimataifa, ambayo watu wengi hiita Jamii na wanaanga “Astronomy Community”. Kitu kinachofanya ionekane kama kuna kijiji fulani ambamo wanaanga huishi pamoja. 

Dokezo: Wanaanga wana fikra kuwa LOFAR itafanikiwa kuvumbua zaidi ya vitu 100,000,000 ambavyo havijavumbuliwa bado na vipo mbali kabisa katika ulimwengu.

Taarifa hii imetokana na ASTRON press release.

Kujinasua na Wingu la Kizingiti Angani

Katika filamu, mashujaa na maadui hurushwa kuelekea mbele baada ya kutokea mlipuko. Hii ni kwa sababu mawimbi makubwa ya nishati ya nguvu, yajulikanayo kama nguvu mtikisiko (shock wave), hutawanywa. Kitu hicho hicho hutokea angani wakati nyota inapolipuka, katika kile kinachoitwa mlipuko wa supanova (supernova explosion).

Nguvu mtikisiko kutoka katika supanova husharabiwa katika mzingo wa nje wa nyota uliojaa gesi na vumbi, ambazo hukimbia kutoka katika nyota kabla ya mlipuko. Nguvu hiyo hupasha joto gesi na kutoa mionzi ya x-ray, ambayo wanaanga wanaweza kuipiga picha kwa kutumia darubini (telescope) maalum zilizopo angani kama picha hii mpya uionayo.

Wanaanga wamepiga picha hii ingaayo ya wingu la gesi na vumbi, ambayo ilichukuliwa kwa tofauti ya takribani mwaka mmoja. Kwa kulinganisha picha hizi mbili za x-ray, wanaanga wanafikiri kuwa nguvu mtikisiko hatimaye ilifanikiwa kujinasua kutoka katika wingu. Hii ni mara ya kwanza kwa wanaanga kuwa na uthibitisho wa x-ray unaoonyesha nguvu mtikisiko (shock wave) ikijinasua kutoka katika wingu la kizingiti cha gesi na vumbi angani!

Dokezo: Nguvu mtikisiko hii iliyotokana na mlipuko wa supanova katika picha umeongeza jotoridi la gesi katika hali ya kustaajabisha ya nyuzi joto 100,000,000 Celsius!

Taarifa hii ya Swahili Space Scoop imetokana na  NASA Chandra X-ray Observatory Press Release.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 78 other followers